Farida alikutana kimwili na Michael wakati ana ujauzito wa miezi miwili. Akamtafuta Michael warudie game Michael akamwambia hayupo amesharudi kazini. Farida akamwambia Michael ana ujauzito na yeye ndo baba wa mtoto. Michael kwa kuwa aliuza mechi kwa Farida akakubali kulea mimba na kodi ya nyumba akaanza kumlipia baby mtarajiwa. Baada ya miezi tisa farida akamwambia amejifungua salama mtoto wa kike. Kumbe alijifungua miezi miwili kabla. Na Mungu analipa hapa hapa duniani Farida akajifungua mtoto ana nywele za kiarabu kuulizwa akasema mtoto amefanana nywele na mama yake Farida. Kaka wa watu akaendelea kumtunza Farida na binti yake mpaka wiki iliyopita alipopata ukweli kuwa Farida amezaa na mwanaume mwingine na alikua anachukua child support kote kote. Michael alimpeleka mtoto kwa mama yake ili ampunguzie majukumu Farida ila alikua anampa Farida mpaka nauli akitaka kwenda kumuangalia mtoto.
Leo Farida kakosa mwana na maji ya moto. Baba mtoto wote wametambua janja yake ya kupokea child support mara mbili . Analia kwa ujinga wake wa kumbambikia mtoto mwanaume aliekua anamsaidia kuliko baba halisi wa mtoto.