Mwisho wa Kiburi ni Anguko!

Salvatory Mkami

Senior Member
Apr 17, 2013
146
244
Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa. Biblia-Mithali 29:23

Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa Bwana; Hakika, hatakosa adhabu. Biblia-Mithali 16:5

Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Biblia-Mithali 16:18

Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. Biblia-Mithali 13:10

Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Biblia-Mithali 11:2

Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; Biblia-Wafilipi 2:3-5

Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Biblia-1 Wakorintho 10:12

Kwa yanayoendelea kutukia wala sishangai kwasababu Neno la Mungu limejitosheleza, hivyo siongezi wala kupunguza neno.
 
Back
Top Bottom