Mwinyi Kazimoto kutua kesho

Mwinyi Kazimoto kutua kesho

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
5.jpg


KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto anatarajiwa kuwasili kesho Saa 1:30 asubuhi kwa ndege ya Qatar Airways, akitokea Qatar anakocheza soka ya kulipwa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba SC na JKT Ruvu, kwa sasa anacheza klabu ya Al Markhiya ya Qatar na anakuja nchini kujiunga na kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji Jumapili wiki hii.
Tayari wachezaji wengine wa nje, washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamewasili nchini leo asubuhi.

Samatta na Ulimwengu wamewasili wakitokea Tunisia ambako Mazembe imeweka kambi ya kujiandaa na mechi za Kundi lake, A Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taifa Stars itamenyana na Msumbiji ‘Mambas’ Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya mchujo, kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.

Wachezaji hao wamefikia hoteli ya Courtyard, iliyopo eneo la Sea View, Upanga mjini Dar es Salaam na leo -watafanya mazoezi kwa programu maalumu waliyopewa na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij wakati wakiwasubiri wenzao watakaowasili kesho kutokea Tukuyu, Mbeya walipoweka kambi.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itawasili Dar es Salaam kesho Saa 3:20 asubuhi kwa ndege ya Fastjet kutoka Mbeya tayari kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Msumbiji.

Katika hatua nyingine, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari keshokutwa kuanzia Saa 5:00 asubuhi kwenye ofisi mpya za shirikisho hilo, katikati ya Jiji.

Chanzo: MWINYI KAZIMOTO ATUA KESHO DAR STARS IKIREJEA KUTOKA TUKUYU, SAMATTA, ULIMWENGU WAANZA MAZOEZI KIVYAO LEO - BIN ZUBEIRY
 
Mwinyi Kazimoto tayari ametua nchini.Kikosi kizima cha Taifa stars kilichokuwa Tukuyu nacho kimetua dar asubuhi kikitokea Tukuyu Mbeya.Jumapili karibuni uwanja wa Taifa tuishangilie Taifa stars!
 
Mh. JAMALI MALINZI, Kitendo cha kupandisha viingilio kutoka 5000 hadi 7000, kimepunguza hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki, hivyo tutarajie kuona mashabiki wachache ambao watakuwa na suport ndogo kwa timu.
 
Mwinyi Kazimoto tayari ametua nchini.Kikosi kizima cha Taifa stars kilichokuwa Tukuyu nacho kimetua dar asubuhi kikitokea Tukuyu Mbeya.Jumapili karibuni uwanja wa Taifa tuishangilie Taifa stars!

Pamoja sana, nitakuwepo...
 
Back
Top Bottom