Mohammed Amiti
New Member
- Mar 2, 2017
- 1
- 6
Habarini wanafamilia,
Utotoni mwangu nilikuwaga hata sinuki lakini nilivyojiunga na shule ya boarding nikaanza kunuka kuanzia form 2. Basi nimekuwa ninanuka mpaka leo nimeishakuwa mtu mzima na ninategemea kuoa. Kazini kwangu hata kabla sijapishana na mtu basi huyo mtu ataanza kuziba pua na kama yuko mbali basi akiniona tu utamwona anatema mate au kuvuta koromeo la koozi kuashiria kwamba anajiandaa kukabiriana na harufu yangu mbaya.
Nimejitahidi sana mpaka kufikia kuzoea ratiba ya kuoga mara 3 kwa siku lakini wapi, nikioga nina kuwa salama kwa masaa mawili ya mwanzo lakini baada ya hapo ninakuwa kero kwa watu. Harufu mbaya inayowatesa wenzangu mimi siisikii lakini wao inawashinda. Nimekuwa nikiharibu siku za watu kila mara.
Sehemu ambayo nimekuja kugundua kwamba inato harufu hii ni kwenye mapumbu (Samahani kwa kutumia lugha kali lakini sina namna ya kuweka tafsida ya hili neno bila kuharibu maana). Nimekuwa nikiosha sana pumbu zangu usiku, mchana na asubuhi lakini haija saidia. Hakuna mtu duniani anayejitahidi kuoga kama mimi. Kuna ndugu zangu wengine anaweza asioge hata wiki lakini mimi nikioga muda huu baada ya masaa 3 ninanuka balaa. Mimi ni mtu mwembamba tu na wala umbo langu sio kubwa na wala sina mafuta mafuta lakini, hii harufu inaninyima raha ya kuwepo duniani.
Mimi ni mpole ukiniona lakini kiuhalisia mimi nilikuwaga mtundu sana na huu upole wangu wa sasa ni siri yangu, upole wangu ni kwa sababu ninanuka kwa hiyo sina amani ya kujitutumua mbele ya jamii inayo nizunguka. Inanibidi niwe mpooooole na tulivu hata muda mwingine nimekuwa mtu wa ndio mzee, sawa mkuu, ilimradi tu kuharakisha mtu asisimame na mimi kwa muda mrefu akaisikia harufu yangu kali akawa ananikimbia kwenye korido. Marafiki zangu wa kweli ambao tumeishi nao muda mrefu mpaka nimefanya pua zao kuzoea harufu yangu na wala hawaoni kama ninanuka, ukiwauliza watakwambia jinsi mimi nilivyo mtundu, mcheshi na mpenda sifa tena machepele kweli kweli dakika mbili mbele, lakini ni kwa hawa tu ambao kwao mimi sinuki bali ni shujaa.
Wadau naombeni msaada sana katika hili ili niweze na mimi kujihisi ni mtu wa kawaida kwa kuondokana na hili tatizo nguli katika maisha yangu.
Natanguliza shukrani zangu kwenu.