Mwili wa muuaji wa watu 9 wapigwa makofi

Mwili wa muuaji wa watu 9 wapigwa makofi

duet

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2013
Posts
534
Reaction score
149
MAZIKO ya mtuhumiwa wa mauaji ya watu tisa na unyang'anyi wilayani hapa, Kichune, yamesuswa na ndugu zake. Tangu Kichune afariki dunia Februari 9 kwa ugonjwa wa pumu katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime, hakuna ndugu aliyefika kuchukua mwili huo.

Kutokana na kukaa mochari kwa muda mrefu na kuharibika, Halmashauri ya Mji ililazimika kusitiri mwili huo kwa kuuzika jana. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Tarime, Dk Michael Nega alisema walilazimika kumzika baada ya kukaa muda mrefu bila ndugu zake kujitokeza.

Imetulazimu kwenda kumzika Kichune kutokana na ndugu zake kuususia mwili mochwari ya hospitali hii na kuharibika na kutoa harufu kali," alisema Dk Nega.

Katika hali isiyo ya kawaida Jumapili iliyopita baada ya kufariki dunia kwa Kichune, mmoja wa wakazi wa Tarime aliyefika kutambua mwili huo, alilia na kuupiga makofi. Mkazi huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja, inadaiwa amefiwa na wajukuu zake wawili, David Yomami na Samwel Richard, ambao wanadaiwa kuuawa na Kichune.

Vijana hao wawili waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wakitengeneza gari lao lililokuwa limeharibika. Kichune alikuwa na majina zaidi ya moja ambapo katika baadhi ya maeneo alikuwa akitambulika kama Josephat Chacha au Charles Msongo

Polisi inadai baada ya kukamatwa, alikiri kuhusika na mauaji ya watu mbalimbali katika kata za Binagi, Turwa na Kitare katika vijiji vya Mogabiri, Kenyamanyori, Nkende na Rebu. Kichune alikamatwa Februari 6 Tanga alikokuwa akifuatiliwa na Polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Baada ya kukamatwa, uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa baada ya mauaji ya watu tisa, alikodi pikipiki kutoka kijiji cha Kenyamanyori alikokuwa akiishi, hadi Musoma. Alipofika Musoma, inadaiwa alihifadhi bunduki aina ya SMG na risasi kadhaa kwa mshirika wake, Marwa Keryoba maeneo ya Bweri na alipokamatwa alimtaja Keryoba kuwa ndiye anayetunza silaha hiyo.

Februari 7, Polisi walifuatilia silaha hiyo kwa Marwa na kumkuta mtuhumiwa, ambaye alitakiwa kujisalimisha lakini alikaidi na kuwarushia risasi askari. "Marwa aliuawa Februari 7 alfajiri maeneo ya Bweri mjini Musoma, alipotakiwa kujisalimisha na kukaidi na kuanza kurushiana risasi na askari," alisema Kamanda Kamugisha.

Source: Habari Leo
 
Acha kusoma habari nusu nusu
 
Cjaelewa!

Kiswahili hicho Mkuu! Ngoja nikutafsirie. Mwili wa (maiti ya) muuaji wa (aliyefanya mauaji ya) watu 9; wapigwa makofi (ulipigwa makofi kuonyesha hasira ya wale waliouliwa ndugu zao).

Lakini usiwe MVIVU, take your time and make a thorough reading of this thread.
 
mi mwenyewe sijaelewa alifariki kwa ugonjwa wa pumu au kupigwa risasi
 
hivi wakurya mna laana ya nani? mbona mnapenda damu za watu hivyo
 
Umauti umekosesha siri ya mauaji yote hayo. Japo polisi inadai kua ni jabazi. Mbn kwengine aliua na hakuchukua kitu?. M/mungu ailaze roho yake inapo stahili.
 
Mtuhumiwa wa mauaji alifariki kwa pumu ila aliyehifadhi bunduki ya huyo mtuhumiwa ndio aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya kurushiana risasi na polisi.
(Kichune na Marwa)
 
Back
Top Bottom