Mwili wa marehemu wafukuliwa upya kwa amri ya mkuu wa wilaya, polisi na daktari wachukuliwa hatua

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,967
19,195
Mwili wa marehemu aliyekuwa mwanafunzi wa sekondari ya Itete wilayani Kilosa mkoa Morogoro Magreth Magwira umefukuliwa baada ya kukumbwa na utata wa kuwa binti huyo ameuawa.

Kifo hicho kilisababishwa na marehemu kuchomwa na kitu cha ncha kali lakini dakatari wa zahanati ya kijiji alisema kifo kilitokana na maradhi ya moyo.
Mkuu wa wilaya ya Kilosa ameamuru daktari na mkuu wa polisi wilaya wachukuliwe hatua kutokana na kuficha sababu ya kifo.

Kama watalaam wanadhalilisha taaluma yao wa adhibiwe tu ila kama kuna mengne nyuma ya pazia basi mungu awape wepesi wataalam wetu
 
Mait imekaa siku ngap chin wasije wakafukuaa wakakuta sehemu ya kitu kuchoma hakipo ila kuna funza tu
 
Mimi ndiyo maana huwa nakua na utata na baadhi ya wafanyakazi wa kada ya kama waganga,halafu mtu mwingine nikitilia mashaka maamuzi ya daktari,eti anasema "daktari ameandika".Kwa dhati kabisa hii fani ya udaktari imevamiwa na wahuni wengi tu ambao wengi wanaprove failure katika utendaji kazi wao.Mimi ntaendelea kuwatilia mashaka popote pale ninapokua na wasiwasi juu ya umahiri wao katika utendaji kazi.Japo nimetoka nje ya mada husika,lakini kiukweli wananchi tuwe tunakua na wasiwasi wa baadhi ya maamuzi ya baadhi ya watumishi.Tusifanyie kazi maamuzi bila kufikiri,unaambiwa mgonjwa amekufa kwa saratani wakati siyo kweli.Wachukuliwe hatua stahki wahusika wote.R.I.P.
 
Mmh!! na wafukuaji nao wameingizwa chaka na Mteule, ina maana hawa wateule hawana washauri!?
Sidhani kama watendaji watatii amri ya mteule na wakifanya hivyo watakua wameingia chaka na itakula kwao vibaya kila mmoja ana taaluma yake hapo,huyo mteule ni mwanasiasa tu akishawaingiza chaka anapata sifa likisanuka anawaruka.
 
Mimi ndiyo maana huwa nakua na utata na baadhi ya wafanyakazi wa kada ya kama waganga,halafu mtu mwingine nikitilia mashaka maamuzi ya daktari,eti anasema "daktari ameandika".Kwa dhati kabisa hii fani ya udaktari imevamiwa na wahuni wengi tu ambao wengi wanaprove failure katika utendaji kazi wao.Mimi ntaendelea kuwatilia mashaka popote pale ninapokua na wasiwasi juu ya umahiri wao katika utendaji kazi.Japo nimetoka nje ya mada husika,lakini kiukweli wananchi tuwe tunakua na wasiwasi wa baadhi ya maamuzi ya baadhi ya watumishi.Tusifanyie kazi maamuzi bila kufikiri,unaambiwa mgonjwa amekufa kwa saratani wakati siyo kweli.Wachukuliwe hatua stahki wahusika wote.R.I.P.
Siku ukifika hospital unavuja damu baada ya ajali maeneo ya huko kwao na ukambiwa ndiyo huyo daktari kaokoa maisha baada ya kupelekwa chumba cha upasuaji.Je utakuwa na maoni gani?
 
Back
Top Bottom