Mwigulu Nchemba, tumia busara utupishe!

Mwigulu Nchemba, tumia busara utupishe!

Sir robby

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2022
Posts
2,393
Reaction score
4,086
Wadau poleni na sekeseke la utitiri wa tozo mbalimbali mnazokumbana nazo chini ya wizara ya fedha chini ya waziri wake bwana Mwigulu mchemba waziri mwenye kauli za kejeli dhidi ya walipa kodi.

Waziri huyu amekuwa mshauri mbaya kwa mheshimiwa Rais kwani amekuwa hana uwezo wa ubunifu wa vyanzo vya mapato visivyo muumiza maskini mwananchi wa nchi hii.

Waziri huyu kwa kinywa chake amekiri kuwa yeye ni binadamu alikosea lakini kukiri kwake hakuna maana kwani aliwahi kuwakejeli walipa kodi kuwa anayeona hawezi kulipa kodi aende burundi bado akadanganya kuwa tozo ni kauli ya wananchi wakati sio kweli kauli hizi ni kuwakejeli kwa walipa kodi.

Hivyo basi tunamwomba bwana Mwigulu Nchemba ajitafakari kwa jinsi watanzania wanavyomlaumu sana kwa hili la tozo na kauli zake kejeli

"Atupishe tu" watenda kazi ni wengi sana.
606282388.jpg
 
Ukishauri ajiuzulu atakausha.

Mshauri RAIS amfurushe Madiluu!!!!
 
Aanze tu kuwapisha ili ile timu yake ya big nini sijui, ife kwa mara ya pili! Hilo sahau. Bado yupo yupo sana tu. Maana kuna mtu anayemjaza upepo bila shaka.
 
Aanze tu kuwapisha ili ile timu yake ya big nini sijui, ife kwa mara ya pili! Hilo sahau. Bado yupo yupo sana tu. Maana kuna mtu anayemjaza upepo bila shaka.
Kuna namna madelu amejichimbia kwenda chini zaidi, maana si kwa kejeli hizi kwa watanzania...
 
Back
Top Bottom