Mwigulu Nchemba: Nimewaelekeza polisi kuwashughulikia vinara wa vurugu na uchochezi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyetaka kujua hatua ambayo serikali inachukua baada ya kubainika kuwa kuna wanasiasa wanahamasisha vurugu na uvunjifu wa amani, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amesema kuwa Serikali haitavumilia kuona mtu ama kundi lolote likihatarisha amani na utulivu wa nchi kwa njia yoyote ile. Amesema kuwa kuna tabia imeanza kujitokeza kwa baadhi ya wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani kutoa matamshi yenye kuchochea vurugu, uvunjifu wa amani na hata umwagaji damu. Amesema kuwa wizara yake kupitia Jeshi la Polisi itahakikisha kuwa vitendo hivyo vinakomeshwa mara moja ili nchi iemdeleee kuwa ya amani

" Mheshimiwa Naibu Spika, nimewaagiza vijana wangu ( polisi) kuwashughulikia wale tu vinara na si kuhangaika na wananchi wasio na hatia ambao wanapelekeshwa tu na wanasiasa hao. Amesema kuwa ipo tabia ya baadhi ya wanasiasa kutoa maneno ya uchochezi na kuwatanguliza wananchi wasio na hatia na pindi jeshi la polisi linapochukua hatua, wanaoathirika ni wananchi hao na si wale waliochochea. Kwa hali hiyo jeshi la polisi limeshabadili mbinu za kupambana na vitendo hivyo na badala yake itashugulika na wale vinara tu" Aliongeza Waziri.

Mytake: Niwapongeze Jeshi la Polisi na Wizara ya Mambo ya ndani kwa kuliona hili. Hii ndio njia muafaka ya kuwatulia hawa wahalifu bila ya kuleta madhara. Naona kazi imeshaanza hasa kwa kuwaita na kuwahoji baadhi ya wanasiasa wa upinzani akiwemo Mbowe, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Ole Sosopi, Kubenea nk. Kazi imeshaanza. Heshima inarudi.
 
Hili lipo sawa Jaman, waandamane wenyewe sasa!
 
wawashuhulikie na majambazi na vibaka mitaani sasa kila siku watu wanauwawa wanaporwa wao wanahangaika na wanasiasa tu.....hii nchi ya hovyo sana siasa zimetuathiri sana
Majambazi na vibaka wanapukutika kila uchwao. Huangalii taarifa ya habari nini? Naiona Tanzania isiyo na ujambazi
 
Nchemba huwa anaongea halafu utendaji wake hamna kitu rejea maazimio ya escrow alipokuwa naibu wazir wa fedha mwisho wa siku maafisa wote wa tra waliohusika kupokea milion 80 hakuna alichowafanya.
 
Hivi Lizaboni huwa una elimu gani make ww huwa unashabikia utumbo tu? Hasa kupigwa kwa Wapinzani!!
Nimefurahi tu waziri wangu kutamka kuwa watashuhhuliwa wale vinara tu. nasubiri kuona mamvi akiswekwa rumande
 
Naona kazi imeshaanza hasa kwa kuwaita na kuwahoji baadhi ya wanasiasa wa upinzani akiwemo Mbowe, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, Ole Sosopi, Kubenea nk. Kazi imeshaanza.

hahahahahahhaha...mnajidanganya sanaaaa...na hapo hata mwaka bado....

subirini mtakapozidi kupoteana...mtakamata na kuhoji hadi vivuli vyenu
 
Hivi nikwann wabunge wa upinzani wanawaumiza sana vichwa mnaacha kujadili maswala ya kitaifa mnawawazia wao tu, mkiwaacha wakapiga kelele zao wakamaliza mtapungukiwa na nini?
 
Back
Top Bottom