Mwigulu Nchemba na Harrison Mwakyembe wamepoteza sifa za kuwa Mawaziri, Unafiki na kuganga Njaa tu!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,729
5,383
Nitangulie kusema mapema kabisa kuwa mimi ni miongoni mwa watu tuliokuwa na imani kubwa na Rais Magufuli na serikali yake pamoja na makosa yaliyokuwa yakifanyika wakati akichukua hatua mbali mbali. NILIMVUMLIA kama ambavyo baadaye akatushauri Dr.Wilbroad Slaa.

Kutokana na mambo ya hovyo na ya aibu yanayoendelea hapa Nchini kwetu kwasasa huku Uchumi ukisuasua NAKARIBIA kusema,endapo hii itakuwa ndiyo "DIRECTION " ya Uongozi wa Rais Magufuli basi mwaka 2020 wana CCM hatuna budi kumpinga Rais Magufuli kwa nguvu zetu zote kuliko Nguvu iliyotumika kumzuia Edward Lowassa kwenda Ikulu. Vinginevyo ataiua CCM!

Mwigulu Nchemba yupo kama hayupo,vijana wa Kitanzania kama akina Roma Mkatoliki wanafanyiwa unyama wa kutisha katika Nchi huru kama hii! INAUMA SANA! Katika Nchi zenye watu makini basi MWIGULU NCHEMBA na HARRISON MWAKYEMBE wangekuwa wamejiuzuru muda mrefu sana!

Tena MWIGULU NCHEMBA acha kabisa kutia watu hasira kwa kujibu utumbo kama ulivyofanya katika thread ulitupiwa na LIZABONI humu JF.Tunajua umeajiri tu-vijana tulivyofeli kama watu wako wa IT wanaoshinda kwenye ACCOUNT zako kukujibia hoja mbalimbali lakini upeo wao ni wa chini sana! Ona sasa walivyokuabisha kwenye majibu yako dhidi ya LIZABONI !

Halafu hata lugha hawajui ona walivyokuabisha Waziri mzima kwenye ile tweet yako uliyotoa kuwa NAPE si muhalifu wala hana rekodi hiyo,badala ya BASTOLA wakakuandikia BASTORA,na hata sasa WELEDI wanaandika WEREDI acha kutumia VI.LA.ZA kwenye mambo ya msingi kama haya ya Nchi! AIBU SANA KWAKO!

Kuanzia issue ya Ben Saanane, Madawa ya kulevya,kuvamiwa kituo cha utangazaji cha CLOUDS media,Nape Nnauye kutolewa bastola na sasa akina ROMA Mkatoliki kutekwa hujaonesha Leadership zaidi ya unafiki na kuganga njaa tu! YUMBISHWA NA MSIMAMO NA SI NJAA by Nape Nnauye.

Mtu mwingine anayetia KINYAA ni huyu HARRISON MWAKYEMBE,ungeona alivyoshiriki na kujibu maswali ya waandishi wa habari katika ile Press conference ya Roma Mkatoliki basi ungejua nini maana ya UNAFIKI na NJAA katika siasa ! Tunajua mipango yake ya kuwa mjasiriamali mkubwa kupitia mradi wake wa Umeme wa Upepo (POWER POOL EAST AFRICA) pale Singida uliDUNDA lakini bado asingekuwa so low vile.NJAA HULETA AIBU SANA!

Hata mjinga ambaye hakwenda shule angejua tu baada ya kumsikiliza ROMA MKATOLIKI ameteswa na watu gani! Ni wale wale waliomtesa ULIMBOKA STEVEN! Kama mtu anabisha basi ni kwanini Zamaradi Kawawa na Mwakyembe walikuwa so defensive vile ! AIBU!

NAPE NNAUYE na HUSSEIN BASHE pambaneni muiokoe CCM watu wengi tuko nyuma yenu na Future yenu ni kubwa kuliko WANAFIKI hawa wanaoganga njaa!

Mwisho Rais Magufuli tunakupenda na kukuheshimu lakini tambua kuwa tulikupa kura zetu uwe kiongozi wetu na si "MUNGU WETU" kubali KUPOKEA USHAURI na pia KUKOSOLEWA vinginevyo come 2020 utachukua FOMU MWENYEWE na safari ijayo UTAJIPIGIA KURA MWENYEWE.

Ahsanteni ngoja niandae zana zangu za kuendea kesho shambani kuna vimanyunyu hapa MWANDUHITINJE ngoja tuvitumie tusije tu-KAFWAAAA!
 
Mwakyembe hana maana kabsaa! , Mwigulu anajua analo lifanya., na ukweli unajulikana kuwa Bashite ndio ana fanya kazi ya Mwigulu, lets say Mwigulu naye katekwa kama Roma hana cha kufanya. ila ukweli ana uona
 
Hawa watu wanafiki sana,utashangaa miaka ijayo mtu kama mwigulu atataka kugombea urais,kama hapa tuu ndo kashindwa hivi je huo urais atauwezea wapi!ni bora kulinda reputation yako kuliko kulinda tumbo lako na hiyo akili iliyohamia tumboni itagharimu your political carreer siku za mbeleni.kama unaona kwenye wizara yako kuna remote control somewhere else na wewe huna usemi unasubiri nini kupisha hicho kiti kwa ujasiri badala ya kukaa kuganga njaa just because unaogopa mkono kutokwenda kinywani endapo utachukua maamuzi sahihi!ukimya wako unakufanya uzidi kuonekana bogus every day,bora hata harison tatizo lake ni la mda mrefu na hana political carreer in the future,lakini wewe.......haya!
 
Huyo mzee wa polonium ni mnafiki na mchumia tumbo tu yani njaa kali,bashite ni kilaza wa std 7 hana akili zaidi ya kutisha watu ili aishi mjini kwa hela za matajiri
 
Mkuu umeongea vitu vya maana sana kama ndugu yang mwigulu anategemea wakina lizaboni kuja kumtetea humu amepotea mana wale ni vilaza sana na jibu zao hoja zimekaa kishabiki na ki udom udom...pili mim mwenyew mwana ccm lakin cwez kushabikia ujinga pale penye maslah ya nchi ko lazima tupinge hili la huyu bwana mdogo kuharib taswira ya chama na kuwafanya wanachama wenzetu waonekane wachumia matumbo sabb wanamuogopa mtto wa mwenyekiti
.
.
.
Kyenekyaka nkighanile une
 
Mi nasemaje mungu wetu halali wala hasikii njaa anatuona na anajua muda utafika na ataamini tu bila kulazimishwa god protect us
 
Back
Top Bottom