Mwigulu Nchemba: Hawa wanaouwa sio Watanzania, ndio maana miili inapookotwa wananchi hawashtuki

mjingamimi, watu hao wanatoka hapa hapa duniani ila:-
  • siyo ndugu zako maana ungeshaenda kuwatambua;
  • siyo kosa la serikali maana lingekuwa kosa lao wasingesema wamewaokota- wangepotezea tu
UNAFIKIRI KUULIWA WATU NI SAWA?
HATA KAMA SIO NDUGU ZAKO?
 
Ww hujaelewa hao wasafirishaji wanaweza tupa popote iyo miili au hujaona ilo lori la hao wahamiaji kwa mwendo huo lazima wafe tu
Na mbaya zaidi dereva hajalimudu baada ya kupoteza muelekeo na kukosekana kwa dira.........wacha wazitupe tuu hizo maiti popote
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba ametahadharisha umma dhidi ya kauli mbalimbali zisizothibitika kuhusu usalama wa raia na mali zao zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Dkt. Nchemba amesema hayo mjini Dodoma katika Mahojiano maalum na Mwandishi wa TBC1 Victoria Patrick ambapo pamoja na mambo mengine ni madai ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa, amesisitiza raia kutoa taarifa kwa vyombo vya dola wanapo hofia usalama wao.

Waziri Mwigulu Nchemba amesema yapo matukio yanayofanyika kwa ajili ya kuchafua taswira ya nchi na ndio maana dot zinazounganishwa ni nyingi mno

Amesema inapotokea miili inaokotwa baharini, bahari ambayo tunachangia na nchi nyingi sana ambayo upepo unaweza kusafirisha miili kutoka sehemu mbali, basi watu wanasema watu wanauawa ovyo

Amesema haiwezi watu wakawa wanauawa hovyo na kukawa shwari kama kulivyo, watu wangepiga kelele kwa sauti

Ameendelea kusema kila tukio linapotokea serikali inachukua hatua na maisha ya watu yanapopotea sio vyema kuhusisha siasa, maana maisha yana thamani sana

ATWAMBIE NA HUYU SI MTANZANIA ???

Hapa ndipo napoaanza kuushangaa uzalendo wa viongozi wetu, hapa ndipo naposhangaa uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu, waziri unajibu hoja ya mauaji as if ni hoja kuchapwa mtoto shule, majibu myepesi kama mtoto wa form two,
Afu huyo jamaa ni PhD holder.... kama elimu ya Bongo inadumaza akili vile?
 
ni kweli...yawezekana wanatoka hizo nchi tunazoshea nao bahari..
ila je kwanini zimetamalaki utawala huu?? na kwanini asiseme ni wa nchi gani sasa?

sielewi ulichoenda kufanya shule wewe.
 
Yaani hilo lichama lina uwezo mkubwa sana wa kuwabadilisha watu kuwa mazombie!
 
Nauliza tu swali...

Hivi kipinde kile MV Bukoba ilivyozama kuna milii yoyote Iliyokutwa/kuokotwa kwenye fukwe ya ziwa?

cc: mahondaw
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba ametahadharisha umma dhidi ya kauli mbalimbali zisizothibitika kuhusu usalama wa raia na mali zao zinazoweza kuhatarisha amani ya nchi.

Dkt. Nchemba amesema hayo mjini Dodoma katika Mahojiano maalum na Mwandishi wa TBC1 Victoria Patrick ambapo pamoja na mambo mengine ni madai ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa, amesisitiza raia kutoa taarifa kwa vyombo vya dola wanapo hofia usalama wao.

Waziri Mwigulu Nchemba amesema yapo matukio yanayofanyika kwa ajili ya kuchafua taswira ya nchi na ndio maana dot zinazounganishwa ni nyingi mno

Amesema inapotokea miili inaokotwa baharini, bahari ambayo tunachangia na nchi nyingi sana ambayo upepo unaweza kusafirisha miili kutoka sehemu mbali, basi watu wanasema watu wanauawa ovyo

Amesema haiwezi watu wakawa wanauawa hovyo na kukawa shwari kama kulivyo, watu wangepiga kelele kwa sauti

Ameendelea kusema kila tukio linapotokea serikali inachukua hatua na maisha ya watu yanapopotea sio vyema kuhusisha siasa, maana maisha yana thamani sana

Mwigulu anatakiwa ajibu swali hili: Kama maiti zilizookotwa si za Watanzania atupe majibu Watanzania waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha ambao hadi leo hawajapatikana wako wapi??
 
Amesema haiwezi watu wakawa wanauawa hovyo na kukawa shwari kama kulivyo, watu wangepiga kelele kwa sauti
Hivi hawa watu sijui ni wagonjwa wa akili...kwa hiyo Mwigulu anaona sasa kuko shwari? Na hajasikia kelele zikipigwa?

Kama kuko shwari kwanini kafanya hiyo interview? Ina maana hata hayo maswali ya mwandishi yeye hajaona kama ni kelele? Kazi ipo
 
Hapa ndipo napoaanza kuushangaa uzalendo wa viongozi wetu, hapa ndipo naposhangaa uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu, waziri unajibu hoja ya mauaji as if ni hoja kuchapwa mtoto shule, majibu myepesi kama mtoto wa form two,
Ulitaka alie machozi kama Linda?
Umeshajiuliza wahamiaji haramu wanaosafirishwa kwa malori kila kona ya Nchi wakiwa wamefungiwa kwenye container wakifa huachwa wapi? Umeona gari iliyokamatwa Leo Dodoma? Ikiwa nao zaidi ya 60 na Carton za maji?
Ni wangapi wameshaenda polisi kutoa taarifa a kupotea kwa watu wao tofauti na hawa wanaojiteka wenyewe kwa msaada wa social Media?
We need to wake up and focus on the productive things and not this political madness
 
Back
Top Bottom