Standalone
JF-Expert Member
- Nov 15, 2014
- 676
- 576
Namheshimi sana Mwigulu kwa uzalendo wake, lakini kuna maswali hapa yananitatiza.
Tunasema kwamba viongozi kama mawaziri wasipokee zawadi kubwa toka kwa wafanyabiashara kwa kuwa zawadi kubwa zinahusianishwa na rushwa
Tibaijuka kawajibishwa kwa kupokea zawadi ya Tshs 1.6 billion toka kwa mfanya biashara.
Iweje basi, kwa Tibaijuka iwe si sawa kupokea zawadi ya Tshs 1.6b, na kwa Mwigulu iwe sawa kupewa zawadi ya huduma ya chopa ya bure na mfanya biashara? Je, tunaelewa thamani ya huduma ya chopa hiyo ikiwa Mwigulu angetakiwa kuilipia kuzungukia mikoa ya Tanzania? Na kama huyo mfanya biashara angempa Mwigulu hizo fedha ili akakodi chopa, ingeonekana ni sawa?
Na huyo mfanya biashara atapata nini toka kwa Mwigulu? Je Mwigulu ataweza kumkatalia chochote atakachodai akijua alifadhiliwa kwa chopa?
Naona tuna tatizo la double standards.[/QU
mkuu mwigulu hana uzalendo wowote ni mganga njaa anayetumia jukwaa la siasa kutafuta umaarufu ni hopless kabisa
Chopa Yenyewe mbona magumashi, EXIT/KUTOKA iko nje. mtu aliye nje anahitaji hayo maelekezo kweli? na mtu akiingilia hapo inakuwaje? hauruki?
hii Chopa rubani wake ni mh. Lembeli?
teh teh teh
Eti Mwigulu mzalendo!upuuzi mtupu,watz wanashawishika na vitu vidogo sana asee
Namheshimi sana Mwigulu kwa uzalendo wake, lakini kuna maswali hapa yananitatiza.
Tunasema kwamba viongozi kama mawaziri wasipokee zawadi kubwa toka kwa wafanyabiashara kwa kuwa zawadi kubwa zinahusianishwa na rushwa
Tibaijuka kawajibishwa kwa kupokea zawadi ya Tshs 1.6 billion toka kwa mfanya biashara.
Iweje basi, kwa Tibaijuka iwe si sawa kupokea zawadi ya Tshs 1.6b, na kwa Mwigulu iwe sawa kupewa zawadi ya huduma ya chopa ya bure na mfanya biashara? Je, tunaelewa thamani ya huduma ya chopa hiyo ikiwa Mwigulu angetakiwa kuilipia kuzungukia mikoa ya Tanzania? Na kama huyo mfanya biashara angempa Mwigulu hizo fedha ili akakodi chopa, ingeonekana ni sawa?
Na huyo mfanya biashara atapata nini toka kwa Mwigulu? Je Mwigulu ataweza kumkatalia chochote atakachodai akijua alifadhiliwa kwa chopa?
Naona tuna tatizo la double standards.
Dr slaa ndo mzalendoÙnasema mwigulu sio mzalendo na ni upuuzi, je kwako wewe kiongozi yupi ni mzalendo?