Mwigulu Nchemba aagwa Iramba Magharibi

Djumbe

Member
Joined
Apr 8, 2011
Posts
39
Reaction score
62
Majigambo na vitisho vingi vya naibu katibu mkuu wa CCM na mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba yalidhihirika kuwa ni kelele za chura baada ya wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya CHADEMA iliyofanyika wiki iliyopita katika vijiji mbalimbali jimboni hapo, Wananchi walidhihirisha kumchoka Mbunge huyo mwenye vituko vya kisiasa visivyowasaidia waliomchagua kwa kulalamikia utendaji wake mbovu jimboni huku wakiorodhesha kero ndogo ndogo alizoshindwa kuzitekeleza ukiacha zile kubwa ambazo wananchi wanafikiri ni Miujiza tuu ndio inyoweza kuwaokoa kama wataendelea kuwa chini ya utawala wa CCM.


Mwigulu kwa kutaka kuivuruga mikutano hiyo alianza kwa kuwatishia wananchi wasihudhurie mikutano na akaanzisha Ligi ya mpira wa miguu kila tulipokwenda, lakini vijana waliendelea kuja kwenye mikutano yetu na wale ambao walichukua kadi za CHADEMA aliwatoa kwenye Ligi hiyo kama alivyofanya katika kijiji cha Ndulungu.

Nia yake ya kutufanyia fujo ilishindakana kutokana na mikutano yetu yote kupewa ulinzi wa askari Polisi wasiopungua 10, na hivyo wananchi walipata ujasiri wa kuhudhuria na kueleza wazi kero zao.



Katika kijiji cha Tyegelo ambapo kuna umaskini mkubwa sana wa kipato,wananchi walilalamikia kwa uchungu hatua ya Mbunge huyo kutumia Million 13 kuilipa timu ya Simba kucheza mechi Kiomboi siku ya ziara ya Dr Slaa ili kuvuruga mkutano huo ,wakati Dispensary yao iliyoanza kujengwa miaka 3 iliyopita imeshindikana kukamilika kwa kukosekana Sh million 5 tu,huku yeye akiwalazimisha wananchi hao kuchangishana kumalizia ujenzi huo.



Wakati yeye anajitapa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejenga miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara, vijiji vingi jimboni hapo havifikiki kwa gari kikiwepo kijiji cha Makunda (kwao na Mwigulu) pamoja na kijiji alikozaliwa Dr Kitila Mkumbo cha Mgela, huku fedha za mfuko wa maendeleo ya Jimbo anazopewa kila baada ya miezi 3 hazijulikani zinakotokomea na hivyo kusababisha baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kama Emmanuel Edger Ntundu kujitoa kwenye chama hicho na kuhamia CHADEMA kukwepa ufisadi huo.


Pamoja na kuwa ziara yetu tulichagua vijiji na Kata ambazo hazikuwahi kufikiwa na CHADEMA kabla, wananchi walikiri wazi kuwa walifanya makosa kumchagua Mbunge huyo na kwamba hawako tayari kurudia makosa hayo tena 2015, na nilichojifunza mimi ni kwamba wanyiramba huwa hawarudii makosa pale wanapojifunza na kujua ukweli na ndio maana tangu uhuru ni mbunge 1 tu (Nalaila Kiula ) ndiye aliyeweza kulishikilia Jimbo hilo kwa awamu zaidi ya 1.



Tutaendelea kwenda Iramba magharibi kuwaelimisha wananchi ili 2015 ikifika wafanye maamuzi wakiwa na ufahamu wa kutosha na hivyo kutochagua AIBU kama walivyofanya 2010,

na ushauri wangu kwa Mwigulu ni kwamba aanze kufungasha virago vyake badala ya kupoteza muda kwa kutengeneza propaganda dhidi ya CHADEMA ambazo kimsingi zinazidi kuiua CCM na kuipaisha CHADEMA na ndio maana hata hali yake ya kisiasa ndani ya CCM sasa ni mbaya maana hawamhitaji tena na hapo alipo amekalia kuti KAVU.


Mimi nimewasilisha, karibuni mnaojua kubisha maana mnakomaa utafikiri nyie ndo mlikuwepo!!!
 
Maskin mwigulu kachamba weee mwishowe ............!lol

jifunze siasa za kistarabu na za kiundugu na si vita.kijana mdogo ila unanuka damu tu. The hegue inakuita 2016
 
Hongereni kwa kusambaza elimu ya uraia, wananchi wengi siku hizi wanajielewa.

kazi kwa Mwigulu na siasa zake chafu na za kigaidi.!!
 
hivi jamani mwigulu anaonekana mwiba sana kwa cdm, mbona threads za mwigulu haziishi hapa jf, yaan kati ya threads tano zinazoposiwa moja lazima iwe ya mwigulu, jamani watu hawalali kwa sababu ya mtu mmoja, na wangekuwa wawili tz hii ingekuwa je, poleni sana cdm, japo kuwa mnamkuza wenyewe,
 

Hakuna kitu kitakachochangia kunipeleka peponi kama CHADEMA kuning'olea Nchemba.
 
mwigulu familia yake boko dar imemshinda, kampun yake ya mj press inakufa tu, jimboni wanaaza kumuelewa, taifa pia limemuelewa sasa... Anabakisha nini sasa. Tuombe uzima tu, kijana mdogo mambo mengi kuliko uwezo wake, makamanda pingeni kazi lazima 2015 hachomoki tena
 
Teh teh,rais mtarajiwa anaamua hata kuwa toa walio tofauti na chama chake kwenye ligi, sasa akipewa huo urais mbona atalipua watanzania wote wasio wana ccm? Mwigulu huo ubunge ameupata tu kwa sababu ya wananchi wengi wa iramba kukosa elimu ya uraia na umasikini basi! Vinginevyo ubunge angeusikia redioni tu!
 
mwigulu familia yake boko dar imemshinda, kampun yake ya mj press inakufa tu, jimboni wanaaza kumuelewa, taifa pia limemuelewa sasa... Anabakisha nini sasa. Tuombe uzima tu, kijana mdogo mambo mengi kuliko uwezo wake, makamanda pingeni kazi lazima 2015 hachomoki tena.
 
Nawashauri Mwigulu, Nape na Kinana waangalie kesi ya Ruto inavyoendeshwa maana naye ameeanzisha green guard yake. Tunaweka kumbukumbu na vielelezo vyote. Litakapowika akijikuta The Hague hakuna pa kutokea.
 
mkuu mwigulu wangekuwa wawili wangeshaiangamiza tz yetu kuwalipua wafuasi wa upinzani!
 
Waambieni hao watu kuwa Mwigulu hataki tena ubunge bali anagombea urais. Ha ha haa!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
...unajua maana ya kumfungia mtu kazi...wewe subiri tu utaaona siasa ilivyo....
 
Waambieni hao watu kuwa Mwigulu hataki tena ubunge bali anagombea urais. Ha ha haa!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Uraisi wa TFF ndo unamfaa maana anapenda sana ligi
 
mimi nachotaka kusikia ni kwamba kila mkumbo ni mbunge sina muda wa kujadili habari za kupika za mwigulu.


 
unajua mwigulu ni kijana, na vijana wamo humu , halafu ana hasira sasa JF ukileta hasira ujue zitapowa na kwa sasa kapunguza spidi ya kuingia humu baada ya kusakamwa
 
gaidi nchemba kipenzi cha matahira.
upo ndagu au unandaa kikosi kazi cha kwenda kuwamaliza hao vijana wa m4c wanaotoa elimu ya uraia kwa mapanga na mabomu?
naona kichwa kinakuuma eeeeeeh.
utaomba sana poooo safari hii na mbinu zako za kiharamia ktk medani za kisiasa.

Nikuhakukishie tu kuwa kwa elimu yangu ndogo ya sheria lazima nisimame na wewe the Hague huko mbele ya safari kwa kutoa roho za watu na kuwasababishia vilema vya maisha watu wasokuwa na hatia.
unatia kinyaa kama gari la city!!
 
unajua mwigulu ni kijana, na vijana wamo humu , halafu ana hasira sasa JF ukileta hasira ujue zitapowa na kwa sasa kapunguza spidi ya kuingia humu baada ya kusakamwa

Tunapongeza juhudi za walioko mstari wa mbele huko Iramba kuwaelimisha watzn wenzetu. Inatushangaza sana na mara nyingi najuliza ni wananch wenye akili kiasi gani kuwachagua watu Kama nchemba kuwawakilisha.
 
Kama DR. SLAA anavyoonekana mwiba kwa MAGAMBA mpaka mnakosa usingizi Kila dakika hamuishi kimtaja na kumuandika. CHADEMA YATOSHA
 
Taahira kashindwa jimbo sasa anaufikiria uraisi. Lakini akigombea pale mirembe machizi wenzake wanaweza kumpa kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…