Mwigulu na Kitwanga, mlichoagiza kimeshatekelezwa?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Naanza na Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mwigulu Nchemba. Ulipokuwa mkoani Pwani kuzungumza na wadau wa korosho, uliagiza wanunuzi wa korosho kuwalipa wakulima madeni yao. Walipaji wameshalipa? Walipwaji wamelipwa?

Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga, ulipokuwa ukizungumza na maafisa wa polisi pamoja na kuwatembelea, uliagiza kuletewa majina ya wauza madawa ya kulevya. Umeshaletewa? Majina yameshaanza kufanyiwa kazi?

Nitaendelea na wengine kesho. Ngoja niendelee na 'hapa kazi tu!'

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Jitahidi...maana usipoonyesha bidii hiko kidawati chako hapo kwenye korido ya Ufipa atakabidhiwa Sumayi
 
Walikua wanajifurahisha.Maagizo ya Rais mwenyewe hayakutekelezwa sembuse ya mawazir
 
Magu na serikali yake ndani ya CCM ni kelele za chura........
 
Back
Top Bottom