Mwigulu acheza rafu ubunge Iramba

Mwigulu acheza rafu ubunge Iramba

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,521
Amekuwa akitumia wapambe zaidi ya 400 na bodaboda 100 katika kampeni za kura ya maoni. Wagombea wenzake wa Iramba magharibi wakiongozwa na Jairo na Kilimba wamedai anachofanya mwenzao ni kinyume cha utaratibu, so wametishia kususia zoezi la kura kama chama hakitachukua hatua!

Chanzo: Star Tv Habari.

========

Kuna mtu kanitumia hii kwamba Jairo, Killimbah, Gyunda wamegomea mchakato kura za maoni ubunge Iramba, wamemtaka Katibu CCM Wilaya kuacha kumbeba kwa mbeleko Mwigulu Mchemba.

WAKATI zoezi la wagombea Ubunge kujinadi na kuomba kura kwa wananchi likiendele kote nchini ,hali sio shwari ndani ya CCM Wilaya ya Iramba, baada ya wagombea watatu kati ya wanne kutangaza kugomea mchakato wa kura za maoni kwa madai kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba anambeba waziwazi mgombea mwezao Mwigulu Nchemba.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana na kutoa tamko kwa chama Mkoa wagombea hao, David Jairo, Juma Killimbah na Amon Gyunda wamesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na msimamizi wa uchaguzi kura za maoni katika jimbo hilo, ambaye ni Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mathias Shidagisha na msaidizi wake, Mwita Raphael, kuwachezea rafu mbaya.

Jumba Killimbah alidai kuwa mgombea mwenzao Mwigulu Nchemba amekuwa akivunja kwa makusudi kanuni na taratibu za mchakato wa uchaguzi huo huku viongozi wa kamati ya Siasa wakifumbua macho hali hiyo.

"Kanuni za uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Feb 2010, fungu la 3 kanuni ya 17 (v) (1) kimeeleza bayana namna ya kura ya maoni na mikutano mikuu ya kampeni ya matawi itakavyotendeka ambapo inasisitiza wahusika ni wanachama tu." .Alisema na kuongeza;

"Lakini kwa utaratibu usio rasmi, mikutano hiyo jimboni kwetu ni ya hadhara isiyozingatia akidi ya wanachama na kunakuwepo na wanachama kutoka vyama pinzani ambao hushiriki kikamilifu kuuliza maswali kwa wagombea".

Aidha, alidai kuwa msimamizi huyo amekuwa akitumia gari la Mwigulu kusambaza mabango yake hadharani kwenye kata mbali mbali huku akitoa maelekezo kwa makatibu wote wa matawi kuhakikisha Mwigulu anashinda.

"Pia amekuwa akimruhusu mgombea huyo kuambatana na magari yasiopungua 10, pikipiki 100, baiskeli zisizo na idadi na kuhama na wapambe wake kila eneo la mkutano huku akitumia gari kubwa lenye vipaza sauti" alisema Killimbah.

Aidha alidai kuwa Shidagisha amekuwa akidiriki kubariki matusi wanayotukanwa na mgombea mwenzao Mwigulu licha ya kulalamika mra kwa mara lakini Katibu huyo amekuwa akiwataka watwangane wawezavyo mbele ya wapiga kura wao.

Hata hivyo walidai kuwa Mwigulu amekuwa akitumia gari ya umma wa Wizara ya fedha yenye namba za usajili STL 3400 aina ya Land cruiser, gari ambalo alitumia siku ya kuchukua fomu likiwa na namba NW FH.

"Kwa kuwa ni dhahiri msimamizi huyu hawezi kutenda haki na hasa ya kusimamia matokeo ya uchaguzi na kwa kuwa ameshatamka bayana tena kwa viapo na huku akitishia kuwapiga baadhi ya wagombea , sisi kama wagombea tumeonelea tumkatae ndugu Shidagisha na msaidizi wake Mwita Rafael kuendelea kuwa wasimamizi wa uchaguzi Jiimbo la Iramba, sambamba na kuchukuliwa hatua za akimaadili na pia Katibu wa UVCCM Wilaya Abel Makala kuacha kuwa kampeni meneja wa Mwigulu huku akitumia wadhifa wake." Alifafanunua Jairo.

Hata hivyo Killimbah alionesha waandishi wa habari sms inayoonesha kuwa Mwigulu alimtumia mmoja wa wajumbe fedha kiasi cha shilingi laki moja kama njia mojawapo ya kumshawishi kumpigia kura.

Akizungumzia malalamiko ya wagombea hao,Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Aluu Segamba alisema ni kweli yapo na kwamba sekretarieti ya mkoa ilitarajiwa kwenda Wilayani Iramba jana kushughulikia suala hilo.

"Hizi ni changamoto za uchaguzi na hawa ni watu wazima, ni imani yangu tutafikia muafaka maana tutawaita wagombea wote pamoja na kamati ya Siasa ya Wilaya ili tumalize tatizo hili haraka iwezekanavyo.". Alisema Segamba.
 
Wajiunge na ukawa ili mbinu ya tukose wote ifanye kazi vizuri maana huyu jamaa toka atupe ile bajeti mbadala ya upinzani yaani sitakagi hata kumsikia.
 
Anekuwa akitumia wapambe zaidi ya 400 na bodaboda 100 katika kampeni za kura ya maoni. Wagombea wenzake wa iramba magharibi wakiongozwa na Jairo na Kilimba wamedai anachofanya mwenzao ni kinyume cha utaratibu, so wametishia kususia zoezi la kura kama chama hakitachukua hatua! source Startv Habari.
Mijitu haina aibu inaongozwa na shetani. Moral authority Jairo anaipata wapi ya kuchukia maovu! Shetani mkubwa
 
Anekuwa akitumia wapambe zaidi ya 400 na bodaboda 100 katika kampeni za kura ya maoni. Wagombea wenzake wa iramba magharibi wakiongozwa na Jairo na Kilimba wamedai anachofanya mwenzao ni kinyume cha utaratibu, so wametishia kususia zoezi la kura kama chama hakitachukua hatua! source Startv Habari.

Hizo ndio harakati za kurudi mjengoni akili ya ziada lazima itumike
 
Wasijali atakatwa tuu, kama hafuati taratibu za chama, kile kiwembe kilichotumika kumkata kwenye ugombea wa urais kitampitia kwa mara ya pili.
 
Jairo ujanja wake wote ameshindwa na huyu jambazi Mwigulu kutoa rushwa? hizo pesa alizoiba wakati alipokuwa Katibu mkuu wa wizara zimeenda wapi. Kweli ccm bila ya rushwa hupati uongozi. chama cha wahuni sio chama wa wakulima na wafanyakazi ni cha wafanyabiashara
 
Kwanza yeye mwigulu si alisema arudi tena kugombea ubunge...anarud kutumikia chama !! sasa imekuwaje sasa???
 
Jairo ujanja wake wote ameshindwa na huyu jambazi Mwigulu kutoa rushwa? hizo pesa alizoiba wakati alipokuwa Katibu mkuu wa wizara zimeenda wapi. Kweli ccm bila ya rushwa hupati uongozi. chama cha wahuni sio chama wa wakulima na wafanyakazi ni cha wafanyabiashara

Chama cha wahuni ni kile ambacho kiongozi wake amapewa bil.10 kama hongo ili amkaribishe fisadi.

www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/889671-mbowe-amkaribisha-rasmi-lowassa-chadema-43.html#post13396149
 
Hata hapa JF Mwigulu kesha cheza faulu kwa kuja na ID yake nyingine na kusema wagombea wenzake wamejitoa baada ya kuona Mwigulu ni maji marefu. Shida sana Mwigulu.
 
Kuna mtu kanitumia hii kwamba Jairo, Killimbah, Gyunda wamegomea mchakato kura za maoni ubunge Iramba, wamemtaka Katibu CCM Wilaya kuacha kumbeba kwa mbeleko Mwigulu Mchemba.

WAKATI zoezi la wagombea Ubunge kujinadi na kuomba kura kwa wananchi likiendele kote nchini ,hali sio shwari ndani ya CCM Wilaya ya Iramba, baada ya wagombea watatu kati ya wanne kutangaza kugomea mchakato wa kura za maoni kwa madai kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba anambeba waziwazi mgombea mwezao Mwigulu Nchemba.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana na kutoa tamko kwa chama Mkoa wagombea hao, David Jairo, Juma Killimbah na Amon Gyunda wamesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na msimamizi wa uchaguzi kura za maoni katika jimbo hilo, ambaye ni Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mathias Shidagisha na msaidizi wake, Mwita Raphael, kuwachezea rafu mbaya.

Jumba Killimbah alidai kuwa mgombea mwenzao Mwigulu Nchemba amekuwa akivunja kwa makusudi kanuni na taratibu za mchakato wa uchaguzi huo huku viongozi wa kamati ya Siasa wakifumbua macho hali hiyo.

“Kanuni za uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Feb 2010, fungu la 3 kanuni ya 17 (v) (1) kimeeleza bayana namna ya kura ya maoni na mikutano mikuu ya kampeni ya matawi itakavyotendeka ambapo inasisitiza wahusika ni wanachama tu.” .Alisema na kuongeza;

“Lakini kwa utaratibu usio rasmi, mikutano hiyo jimboni kwetu ni ya hadhara isiyozingatia akidi ya wanachama na kunakuwepo na wanachama kutoka vyama pinzani ambao hushiriki kikamilifu kuuliza maswali kwa wagombea”.

Aidha, alidai kuwa msimamizi huyo amekuwa akitumia gari la Mwigulu kusambaza mabango yake hadharani kwenye kata mbali mbali huku akitoa maelekezo kwa makatibu wote wa matawi kuhakikisha Mwigulu anashinda.

“Pia amekuwa akimruhusu mgombea huyo kuambatana na magari yasiopungua 10, pikipiki 100, baiskeli zisizo na idadi na kuhama na wapambe wake kila eneo la mkutano huku akitumia gari kubwa lenye vipaza sauti” alisema Killimbah.

Aidha alidai kuwa Shidagisha amekuwa akidiriki kubariki matusi wanayotukanwa na mgombea mwenzao Mwigulu licha ya kulalamika mra kwa mara lakini Katibu huyo amekuwa akiwataka watwangane wawezavyo mbele ya wapiga kura wao.

Hata hivyo walidai kuwa Mwigulu amekuwa akitumia gari ya umma wa Wizara ya fedha yenye namba za usajili STL 3400 aina ya Land cruiser, gari ambalo alitumia siku ya kuchukua fomu likiwa na namba NW FH.

“Kwa kuwa ni dhahiri msimamizi huyu hawezi kutenda haki na hasa ya kusimamia matokeo ya uchaguzi na kwa kuwa ameshatamka bayana tena kwa viapo na huku akitishia kuwapiga baadhi ya wagombea , sisi kama wagombea tumeonelea tumkatae ndugu Shidagisha na msaidizi wake Mwita Rafael kuendelea kuwa wasimamizi wa uchaguzi Jiimbo la Iramba, sambamba na kuchukuliwa hatua za akimaadili na pia Katibu wa UVCCM Wilaya Abel Makala kuacha kuwa kampeni meneja wa Mwigulu huku akitumia wadhifa wake.” Alifafanunua Jairo.

Hata hivyo Killimbah alionesha waandishi wa habari sms inayoonesha kuwa Mwigulu alimtumia mmoja wa wajumbe fedha kiasi cha shilingi laki moja kama njia mojawapo ya kumshawishi kumpigia kura.

Akizungumzia malalamiko ya wagombea hao,Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Aluu Segamba alisema ni kweli yapo na kwamba sekretarieti ya mkoa ilitarajiwa kwenda Wilayani Iramba jana kushughulikia suala hilo.

“Hizi ni changamoto za uchaguzi na hawa ni watu wazima, ni imani yangu tutafikia muafaka maana tutawaita wagombea wote pamoja na kamati ya Siasa ya Wilaya ili tumalize tatizo hili haraka iwezekanavyo.”. Alisema Segamba.
 
Back
Top Bottom