Mwigamba na Dkt. Slaa kuna nini?

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Nimeisoma kwa umakini makala ya Samson Mwigamba kwenye gazeti la Tanzania Daima la Jumatano Aprili 04, yenye Kichwa cha Habari Ushindi wa Arumeru Mithili ya Operesheni ya Kijeshi imenisikitisha sana.

Ameandika kwa kina mikakati iliyotumika hadi kuupata ushindi huo wa Arumeru kwa kweli makamanda walijituma sana na kuhakikisha kinaeleweka.Ni mikakati inayopaswa kutumika kwenye chaguzi zote.

My Take:
Hata hivyo, katika makala hiyo Bw. Mwigamba kawashukuru makamanda wote kwa majina na jinsi walivyoshiriki kuleta huo ushindi hadi wale alisoma nao shule ya msingi lakini hakulitaja jina la Dkt. Wilbrod Slaa hata sehemu moja.

Mwigamba, hakutambua kabisa uwepo wa Dkt. Slaa kwenye kampeni hizo na kwa kweli imezidi kuleta picha kuwa tuhuma zilizokuwa zinatolewa humu jamvini na akina Tuntemeke zilikuwa na mkono wake..
 
Mmeanza tena kuleta uchonganishi,hakuna uhasama wowote kati ya Mwigamba na Dr Slaa, iacheni CHADEMA Ijiandae kuchukua tena jimbo lake la Arusha
 
Back
Top Bottom