desmond JJ
Member
- Jul 6, 2012
- 56
- 28
Pamekuwa na malalamiko mengi ya viongozi wetu wa juu, kuhusu kuingilia maamuzi ya wananchi katika ngazi za chini (ambao kimsingi ndio mtaji wa chama). Sipingi swala la kuingilia maamuzi hayo lakini namna mnavyoingilia hayo maamuzi au matakwa yetu sisi wananchi kwangu na wengine wengi tu naona kuna walakini,wacha turudi kwene historia ya kipindi Kifupi kilichopita, tulianza kwene uteuzi wa watia nia katika majimbo, yako baadhi ya maeneo mlipuuza maoni yetu, au hamkuwajibika ipasavyo kiasi cha kutuumiza, (mf. Kesi ya jimbo la segerea, ingawa ni uzembe wa wana UKAWA lakini ukweli ni kwamba chadema ndio imechangia kiasi kikubwa kushindwa kwa ukawa hapa M. Kiti wangu na timu yako hamkuwajibika ipasavyo) na maeneo mengine mengi tu palikuwa na shida kama hiyo. Tukayavumilia na kuendelea kulisongesha gurudumu letu la MABADILIKO Tulifanya kazi bila kinyongo, na naamini tulimaliza vizuri.
Tukaja uteuzi wa viti maalum, hapo mmetuwekea sarakasi ambazo kwakweli ni utii na uvumilivu wa hali ya juu wa wanachama ndio ukapunguza malalamiko, na nyie viongozi wa juu wala hamkujali hilo, najua unafahamu kwamba majina mengi ya viti maalum (ubunge na udiwani) katika maeneo mengi yametoka mfukoni, M. Kiti wangu taarifa hizi unazo Mfano Tarime mjini (udiwani) ni dhahiri majina yaliyopendekezwa na kamati kuu ni ya mfukoni sio mapendekezo wala matakwa ya wanachama. Lakini wanachama watiifu tukavumilia. Limekuja swala la uchaguzi wa wenyeviti wa halmashauri na mameya, na hapa nitazungumzia Tarime Mjini ambako uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri umefanyika tarehe 16/12 /2015 baada ya kuendeleza utaratibu ule ule wa majina ya mfukoni badala ya kuacha wenye mji wachague wamtakaye hasa ukizingatia wao ndio wanaoongozwa wewe haupo huku na swala la maendeleo kwa wananchi ni jambo la kushirikiana na wananchi wenyewe, na baada ya mvutano mrefu Kati yako wewe M. Kiti wangu wa chama Mh. Freeman A. Mbowe na viongozi wangu wa chama hapa Tarime juu ya Nani awe Mwenyekiti wa Halmashauri,mwenyekiti ulitamka kauli za kukera(ambazo kwangu hazikuwa na busara) wacha nikukumbushe kauli yako ya KUUDHI moja tu, uliyoitoa kwetu, nikiwa naisikia "Chadema bila Tarime, inawezekana" hiyo ni moja tu Kati ya maneno mengi ya kuudhi uliyoyasema katika mvutano huu kupitia simu yako kwa viongozi wa chama Wilaya. kwangu binafsi hii ni dhihaka, na ni fedheha, pamoja na nguvu kubwa ya kukitafutia kura chama tuliyoitumia sie wanachama Leo thamani ya nguvu zetu haipo tena mbele ya uso wako, nina hofu kesho utasema pia chadema bila Arusha, Dar es salaam, Iringa, Mbeya, Zanzibar na kwingineko inawezekana.
Nakuasa Mwenyekiti pamoja na kwamba unayo mamlaka ya kuwatumikia watanzania, ni vyema ukaziheshimu hisia na mawazo yao, inawezekana uliyoyapendekeza yalikuwa na manufaa lakini ilikuwa bora zaidi kushauri kwa vigezo na sifa ulizoletewa badala ya kutoka na maamuzi ya moja kwa moja, wananchi ndio wanayoyaelewa zaidi mazingira yao na watu wenye msaada kwao
Ni matumaini yangu, unaikumbuka ajenda kuu na ya msingi ya chama, malengo makuu ya chama. Matumaini ya wanachama juu ya chama Chao ni kuona mambo haya yanatekelezwa kupitia viongozi wao waliowachagua. Ni hayo tu Mwenyekiti.