Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohammed Ali Kawaida, amepongeza msimamo thabiti wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka wazi na kwa uwazi mkubwa kupinga jitihada zozote kutoka ndani au nje ya nchi zinazolenga kuchochea chuki na kuharibu mshikamano wa kitaifa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza leo Ijumaa, wakati wa kikao rasmi cha Baraza Kuu la UVCCM kilichofanyika katika Ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, Kawaida amesema kuwa msimamo wa Rais umekuwa ni dira ya vijana wa chama hicho na unathibitisha dhamira ya kulinda tunu ya amani, umoja na mshikamano wa taifa.
Aidha, Kawaida ametoa wito kwa mataifa jirani, yakiwemo Kenya na mengineyo, kuelewa kwa kina hali halisi ya Tanzania na kuunga mkono juhudi za kudumisha utulivu wa kikanda. "Tunawapenda sana majirani zetu, lakini jirani asiye na adabu hawezi kukaribishwa katika eneo letu la usalama," aliongeza.