Mwenyekiti wa Serikali za mitaa katika usuluhishi wa ugomvi kati ya mume na mke

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Mwenyekiti Wa Serikali Za Mitaa


Jamaa alienda kwa Mwenyekiti wa serikali za mitaa kupeleka mashtaka yake,

JAMAA: Mke wangu hataki kunipa unyumba hebu ongea naye kabla sijafanya kitu kibaya, nimekuja naye yuko hapo nje.

MWENYEKITI: Hebu mwite, we kaa nje ya ofisi niweze kumsikiliza.

JAMAA: Poa mkuu

MWENYEKITI: Haya mama kunani tena huko mzee unamnyima unyumba?

MKE: Asubuhi naondoka nyumbani sina senti tano nachukua kibajaji mpaka kazini nikimwambia dereva wa kibajaji sina hela, ananiuliza sasa utanilipa badae au? Mimi nakubali au. Nakuwa hapo nimechelewa kazini, nikifika huko bosi anasema sasa umechelewa nikufukuze kazi au? Mimi nachagua au, jioni narudi nyumbani tena mwenye kibajaji ananiuliza unalipa au? nakubali au, sasa nakuwa nimechoka mzee akitaka namnyima.

MWENYEKITI: Dah! Hiyo stori ya kusikitisha, sasa tumwambie mumeo au?

Hihihihihihihihihiiiiiii! Safari moja huanzisha nyingine!
 
Back
Top Bottom