Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha apandishwa kizimbani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha,Noah Lembris na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kwa tuhuma za kujeruhi na kuharibu mali.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Gwanta Mwankuga na kusomewa mashtaka yanayowakabili katika kesi namba 83 na 84 za mwaka 2016 .

Pamoja na Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ambaye ni Diwani wa Kata ya Oltumet kupitia CHADEMA, watuhumiwa wengine ni William Samwel,Rafael Ngosira,Loserian Solomon na Lucas Lairumbe.

Akisoma mashtaka hayo,Mwanasheria wa Serikali Riziki Riziki alidai mahakamani hapo kuwa mshatakiwa wa kwanza Noah Lembris na Wiliam Samweli kwa pamoja Septemba 27, mwaka jana katika eneo la Olorien wilayani Arumeru walidaiwa kuchoma moto nyumba ya mkazi wa eneo hilo Peter Kambey.

Katika shtaka la pili linalowakabili watuhumiwa wote inadaiwa Februari 29, mwaka huu wanadaiwa kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili Peter Kambey wakati akiwa shambani kwake na kumsababishia maumivu makali.

Watuhumiwa wote walikana mashtaka yanayowakabili na waliachiwa kwa dhamana hadi Aprili 14, mwaka huu ambapo kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo. Awali kabla ya kupandishwa mahakamani na kusomewa mashtaka hayo, watuhumiwa hao walikuwa katika mgogoro wa kugombea shamba lenye ukubwa wa ekari 6 mali ya ajuza Ndetiai Megaro (84) mkazi wa kijiji cha Ilkiushi wilayani Arumeru.

Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka 12 unatokana na baadhi ya viongozi wa kisiasa akiwemo Mwenyekiti Lembris kujaribu kudhulumu shamba hilo kwa kuhamisha umiliki kutoka kwa bibi huyo na kudai kuwa ni eneo la kijiji cha Ilkiushi.


Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom