Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya mjini apigwa risasi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Habari kutoka Jijini Mbeya, zinasema kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya mjini, Ndugu Ephrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka (60) amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29. 01. 2017 majira ya saa 05. 45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwele, Tarafa ya Ntebela, wilayani Kyela Mkoa wa Mbeya

Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala Kitandani nyumbani kwake Ntebela, ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za goroli

Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na hali yake inaendelea vizuri

Kamanda Lukula, amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kumuua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea
111c0781ad66eba9951997ea5e400d48.jpg
Kulia ni Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya ndugu Lobe Zongo akimpokea Mwaitenda katika hospitali ya rufaa Mbeya wakati alipofikishwa hospitalini hapo
241a4876f4cf4bce1061004a900ac842.jpg
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya mjini ndugu Ephrahim Mwaitenda akifikishwa hospitalini hapo

Chanzo : East Africa TV.
 
Hiyo sio habari hukupaswa kuileta..
Hata kama sabbau ya kupigwa Risasi haijafahamika ila Atleast ungesema alipigwa akiwa wapi anafanya nini.?
 
Back
Top Bottom