Mwenyekiti UVCCM, Kheri James: CCM itaendelea kutawala sana

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
UVCCM.jpg
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Taifa UVCCM, Kheri James amesema haitoweza kuja kutokea Chama cha Mapinduzi 'CCM' kutolewa madarakani katika chaguzi zozote zile kwa madai watanzania wa sasa wanaakili sana katika kuamua mambo yao hasa kwenye uchaguzi

Kheri ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri wakati alipokuwa anajibu swali la miongoni mwa mashabiki zake waliotaka kufahamu kwamba je itakuja kutokea siku chama cha Mapinduzi kitashindwa kushinda katika uchaguzi mkuu na upinzani kuchukua madaraka.

"Kwa kipindi hiki ambacho watanzania wana akili timamu sidhani kama CCM itaweza kuanguaka madarakani. Watanzania wana akili sana na wanaiona kesho kubwa ya nchi hii na usalama wa Tanzania bado upo kwenye chama cha Mapinduzi. Hatuzui wapinzani lakini kwa dola ni CCM tu itaendelea kutawala sana", amesema Kheri.

Kwa uapande mwingine, Kheri amesema kumekuwepo na wanasiasa wengi wanaingia kwenye uwanja huo kwa kufuata mkumbo na kuacha misingi ya kisiasa ambayo ni kuzungumza kwa hoja zilizokuwa na tija kwa jamii pamoja na taifa.

Chanzo: EATV
 
Chadema wangekuwa hawana udini na ukabila wangeshachukua nchi siku nyingi saaana!
 
Sio kwa sababu watanzania wa sasa wana akili, ni kwa sababu watanzania wengi bado ni wajinga na ccm pamoja na wanufaika wa serikali yake imefanikiwa kwa kiwango kikubwa so far ku explore huo ujinga. ...
Hata hivyo ni ujinga pia kujiaminisha kuwa CCM haitokuja kung’oka
 
Ukweli mtupu. Na bahati mbaya sana huwa hawakubali. Yaani palipo na mkasikazini hata kama yuko magharibi aidha awe mfanyakazi au Biashara mara nyingi utakuta ni mwanachama wa CDM. Hili jambo lilishawashtua wengi sana. Hata walipomweka boya Mashinji ili eti kubalansi ukanda lkn haikusaidia kwani bwanakaka yupo pale kama pulizo tu wenye nalo akina mdee, mbowe, mtei, lema, mrema, na ndresa. Siku wakifumua mfumo wa namna yakupata uongozi wanaweza kuchukua miaka kumi hadi 15 kuchukua dola. Ila kwa uzito wa uncle Magu mabegani kwao watasubiri sana
Mi nasema hivyo sbb niliona kwa mbunge flani muislam na sio mangi walikuwa hawamtaki kbs ila walimuacha sbb alikuwa anakubalika na raia.jamaa waache udini na ukabila ndio watachukua nchi kilaini.CCM hiyo hawana unaweza kukuta mpare mbunge sumbawanga huko!ila sijui kwa serikali ya sasa kama nyadhifa za juu wanachukua watu kabila mbalimbali.na CCM wakianza ukabila bora tuwatimue tuongoze nchi wananchi wenyewe tuu
 
Ukweli mtupu. Na bahati mbaya sana huwa hawakubali. Yaani palipo na mkasikazini hata kama yuko magharibi aidha awe mfanyakazi au Biashara mara nyingi utakuta ni mwanachama wa CDM. Hili jambo lilishawashtua wengi sana. Hata walipomweka boya Mashinji ili eti kubalansi ukanda lkn haikusaidia kwani bwanakaka yupo pale kama pulizo tu wenye nalo akina mdee, mbowe, mtei, lema, mrema, na ndresa. Siku wakifumua mfumo wa namna yakupata uongozi wanaweza kuchukua miaka kumi hadi 15 kuchukua dola. Ila kwa uzito wa uncle Magu mabegani kwao watasubiri sana
Vyombo vya dola ndio vinavyowasaidia, kubambikia kesi, kuua, kuchinja chinja watu, wizi wa kura, kugaragaza katiba, lakini kama mtakwenda kwa haki bila hivyo vipengele hapo juu, mbona mapema tu mnang'oka,
 
Ameshindwa bwana yule aliye kuwa anajua anakuwa mbunge sasa wataweza hawa vifaranga nya njiwa
 
yaani mnaisema Chadema na ukabila na ukanda ,mnasahau bwana yule tangia achaguliwe anadhania CHATO ndio Tanzania,kweli ukipenda chongo utaita makengeza,SMH
 
Kwa Mimi nimemwelewa,

CCM itaendelea kutawala, ni kauli halisi ambayo nilipenda kuisikia vinywani mwa wamaccm, kutawala si kuongoza, wanatawala.

Safi, watanzania ni watawaliwa hatuongozwi, na CCM inatawala si kutuongoza, Nashukuru Sana
 
Ukweli mtupu. Na bahati mbaya sana huwa hawakubali. Yaani palipo na mkasikazini hata kama yuko magharibi aidha awe mfanyakazi au Biashara mara nyingi utakuta ni mwanachama wa CDM. Hili jambo lilishawashtua wengi sana. Hata walipomweka boya Mashinji ili eti kubalansi ukanda lkn haikusaidia kwani bwanakaka yupo pale kama pulizo tu wenye nalo akina mdee, mbowe, mtei, lema, mrema, na ndresa. Siku wakifumua mfumo wa namna yakupata uongozi wanaweza kuchukua miaka kumi hadi 15 kuchukua dola. Ila kwa uzito wa uncle Magu mabegani kwao watasubiri sana
Ujinga ukizidi kipimo hujenga hoja kwa hisia
 
Back
Top Bottom