Mwenyekiti mpya CHADEMA kupatikana Desemba 13

Mwenyekiti mpya CHADEMA kupatikana Desemba 13

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza ratiba ya uchaguzi wake wa ndani, inayoonyesha kuwa kitapata mwenyekiti mpya ifikapo Desemba 13, mwaka huu. Ratiba iliyotolewa na chama hicho Dar es Salaam jana imeeleza kuwa uchaguzi huo wa mwenyekiti, utatanguliwa na chaguzi nyingine za ngazi za majimbo, mkoa, wilaya, kata na tawi.

"Uchaguzi utaanza Aprili, mwaka huu na tunatarajia umalizike Desemba mwaka huu kwa kumchagua mwenyekiti taifa," alisema Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika. Alisema kuanzia Aprili hadi Septemba kutafanyika chaguzi katika ngazi za msingi ambazo zinajumuisha matawi, majimbo na wilaya kabla uchaguzi huo haujafanyika katika ngazi ya mkoa kuanzia Novemba.

"Uchaguzi ngazi ya taifa utahusisha pia jumuiya za chama ambazo ni Baraza la Wanawake CHADEMA (BAWACHA), Baraza la Vijana (BAVICHA), Wazee, Kamati Kuu na Baraza Kuu Taifa," alisema.

Nafasi nyingine zitakazoshindaniwa ni za wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa.

WEWE KAMA MWANA CHADEMA KINDAKINDAKI UNGEPENDA NAFASI HIYO IPOKELEWE NA NANI?
 
Kamanda Mbowe hagombei tena? Na vp akigombea akashinda atakuwa mkit mpya au?
 
mwenyekiti ajaye inabidi awe jasiri kama mbowe(kama mbowe hatachaguliwa tena)
 
Mbowe msimamo wake upo pale pale au.Manake alishasema hata gombea tena tuanze kuangalia sura zingine
 
Kikubwa anatakiwa mwenyekiti jasiri mwenye kutanguliza maslahi ya taifa zaidi kuliko yale ya chama na mwenye 'uthubutu? Haijalishi awe mbowe au mwingine!
 
asigombee ila angalau kuondoa ule ukabila, ukanda na udini. mind that sijataja kabila, ukanda wala dini ya mtu. I'm too general kwa yasemwayo huku uswazi.
 
maoni yangu mbowe aendelee lakini kama katiba inaruhusu bado nina imani na mbowe hapa chadema wawe makini sana na uteunzi huu wa nafasi muhimu kuelekea 2015 maana kamwe mkimchagua ndumilakuwili hakika ccm watachukulia advantage ya kumkamata huyo jamaa kwa njaa zake na ccm kushinda kirahisi lazima majina yapitiwe vizuri wasichague wenye njaa ya pesa maana atarubuniwa na magamba, apatikane mtu jasiri, mwaminifu wa kuweza kukisogeza chama hapa kilipo na kuendelea mbele,
 
mi pia naunga mkono kamanda mbowe aendelee ni makini sana na magamba wanamuogopa kweli na yupo kwenye record nzuri mpaka sasa

mbowe bado tunamhitaji sana, tafadhali kamati kuu mtisaidie kumuomba mbowe
 
Kamanda Mbowe bado tunakuhitaji hapa tulipo cc ni zaidi ya swala tuliozungukwa na Simba wenye njaa yaani ukithubutu kutuacha sekunde moja utakuja kuta mifupa tu...
Umetutoa mbali na hata sasa tumeshaanza kuyaona majengo na miti ya upande wa pili lakini c rahisi sana kupafikia bila kua na uongozi imara vinginevyotutaishia kua chakula ya Mamba.
Tunaijua dhamira yako ni nzuri lakini tafadhari tunaomba utuvushe hapa kwanza mkuu.
 
mbowe apumzike aendelee kuwa mshauri pr safari, zitto au kitila mkumbo wanafaa pia kugombea uenyekiti
 
mbowe apumzike aendelee kuwa mshauri pr safari, zitto au kitila mkumbo wanafaa pia kugombea uenyekiti


Kama katiba ya CHADEMA inaruhusu muhula mwingine, Nadhani MBOWE bado ni muhimili muhimu katika kukuza siasa za ushindani, demokrasia na kuamsha fikra za watanzania kuhusu ushiriki wao katika kulinda na kufaidika na raslimali za nchi kwa mujibu wa katiba ya sasa Ibara ya 27 (1-2).
 
Back
Top Bottom