Mwenyekiti hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti hii imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by banyimwa, Nov 11, 2011.

 1. b

  banyimwa Senior Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wetu wa Kamati ya bunge ya Mambo ya nje uko wapi? Mbona kimya toka ulipotoka Nigeria? Huku nyuma wenzio tumetishiwa nyau na Cameron kwamba fedha zake haziliki mpaka tuhalalishe mapenzi ya jinsia moja. Waziri wa Mambo ya Nje kaongea na kukataa fedha zinazonuka dhambi ya kudhalilisha utu wa mwafrika.

  Sasa tukiwa tunasubiri kauli yako, muda umezidi kusonga na ndipo nikajiuliza, wewe na kamati yako mko wapi katika hili? Unaliunga mkono au mna kigugumizi kama wenzetu ambao wameshikwa na kigugumizi kwa sababu ya nasaba ya chama chao na Cameron na chama chale cha kihafidhina?

  Mwenyekiti ongea kitu kama ulivyofanya kwa suala la Misri na Algeria. Ongea Mwenyekiti!
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nasikia kashachukua advance fasta kwa hiyo hilo aliongelei..
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mwacheni mzee wa watu ana mambo mengi. Huku wanataka kumvua gamba, huku kuna suala la urais wake unaokwenda harijojo na huku anahangaika kujikusanyia zaidi ili aongeze fuko lake la kampeni na kuwamaliza wabaya wake. Muacheni kabisa jamani!
   
 4. T

  Tiote Senior Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmh! Jamani hela hizi haziwezi kuchukulika kama wenye nazo hawajakupima na kuridhika kwamba unakidhi vigezo. Mzee huyu hana sifa hiyo jamani!
   
 5. n

  ndutu Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa kagundua hilo haliwezi kumpa sifa yoyote ya kisiasa kwa sababu haliongezi wapiga kura zake kule kwenye NEC.
   
 6. m

  mudavadi Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa sasa hivi kabadilisha mbinu ya kujisogeza kwa watanzania na huu ni ushauri wa Nabii wake. Sasa ni kuendesha harambee kwa kwenda mbele! Nasikia amealikwa kuchangia harambee ya kanisa la RC.
   
 7. w

  watenda Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na kile kiharusi chake mzee ataweza kweli kumudu kampeni za kuizunguka nchi yote hii. Hapa tutazika rais aliye madarakani na kutuingiza kwenye uchaguzi mpya. Bora Sumaye apige jaramba amvae kabla ya maafa.
   
Loading...