Mwenyekiti APC Claud Gwandu azungumzia sakata la kukamatwa kwa waandishi wa habari na kuachiliwa

Wembe walioutumia kumnyoa Bashite, waugeuze upande wa pili wawanyolee hao Askari.. Wasusie kuandika habari zao zote.. Kwanza ndo itakuwa poa zaidi maana kila siku hao askari wenyewe wanakuja na habari za uongo daily.. Watatuepusha na mengi..
 
Leo Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia mkusanyiko wa watu walioongozwa na Meya wa Arusha kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba kwenye ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Tukio hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Madiwani, Waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa dini (Wakristo na Waislamu) lilifanyika kwenye eneo la shule hiyo ya Lucky Vicent ambapo wakati wakiendelea kuzungumza wakiwa gorofani ghafla waliona Polisi wamefika kwa spidi na kusema watu wote wako chini ya ulinzi.

Baada ya hapo Polisi waliwakamata na kuondoka nao wote wakiwemo Waandishi wa habari wapatao kumi ambapo baada ya kufika kituo cha kati cha Polisi, Waandishi hao waliachiwa huru huku Polisi wakiwaambia hawana shughuli nao bali waliwapa lift tu kutoka kwenye eneo la tukio.

Kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika dakika chache baadae, Polisi walisema alieamuru Waandishi kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni hakufahamu kwamba hao ni Waandishi na kwamba Wanahabari hao hawana kosa lolote na ndio maana waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.

Kufuatia tukio hilo,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imelaani tukio hilo.

"Tulikuwa tunahangaikia wenzetu waachiwe kwanza na hatimaye tumefanikiwa,wameachiwa huru bila masharti yoyote....maelezo ya kaimu RPC yanakera na kuchekesha,na kwa kweli ni kama kejeli....Eti waandishi hawakukamatwa bali walipewa 'lift' na Polisi kuwarudisha mjini wakati walienda na magari yao na yamebaki shuleni Lucky Vincent,ni jambo gumu kueleweka",ameeleza mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Claud Gwandu.

"Awali waliambiwa kuwa wamekamatwa kwa kukutwa kwenye mkusanyiko usio na kibali lakini waliokamatwa ni waandishi 9, meya wa Arusha,diwani mmoja na viongozi wawili wa dini..Hivyo basi,uongozi wa APC,pamoja na kulaani unyanyasaji huo wa wazi kwa .maelezo ya kina kuhusu kukamwaandishi wa habari,utaandika barua ya malalamiko kwa uongozi wa Polisi Mkoa kutaka atwa kwa wanahabari hao na baada ya hapo utachukua hatua stahiki",ameongeza Gwandu.

Katika hatua nyingine meya wa jiji la Arusha,madiwani,walimu,mmiliki wa shule ya lucky Vincent,viongozi wa dini waachiwa huru kwa dhamana kwa masharti kwamba watakapoitajika muda wowote wafike.

Inaelezwa kuwa wamepewa dhamana baada ya polisi kutaka hizo rambirambi zikabidhiwe kituoni hapo ili ufanyike utaratibu mwingine wa kuwafikishia walengwa jambo lililopingwa vikali na meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro.
 
CCM inatia kinyaa, watu hawajui kuongoza kwenye diversity, halafu katibu mwenezi wao sijui ndio alidumaaga akiwa mdogo, yaniii!
 
NAOMBA KUTOA TANGAZO: KUANZIA SASA NA KUENDELEA MTU YEYOTE ANAYETAKA KUTOA RAMBI RAMBI YAKE KUTOKANA NA MAAFA YATAKAYOTOKEA MAHALI POPOTE KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, AJIHADHARI, ASITOE MCHANGO WAKE KUPITIA OFISI YOYOTE YA SERIKALI IWE YA TAIFA, MKOA, WILAYA, KATA, KIJIJI AU MTAA. HII NI KWA SABABU MICHANGO HIYO HAITAWAFIKIA WALENGWA WALIOPATA MAAFA. HII NI KWA KUWA SERIKALI HUAMUA KUTUMIA MICHANGO HIYO KWA MAKUSUDI MENGINE KINYUME NA DHAMIRA YA MSAADA.
KWA KUWA WATOA RAMBI RAMBI WANATOA KWA HIYARI YAO BILA KULAZIMISHWA NA MTU, HAKUNA ALIYE NA HAKI YA KUWALAZIMISHA KUTOA KUPITIA OFISI YAKE!!!
 
Leo Arusha kumetokea tukio la Polisi kuvamia mkusanyiko wa watu walioongozwa na Meya wa Arusha kwenda kutoa rambirambi kwa familia zilizopata msiba kwenye ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Tukio hilo ambalo pia lilihudhuriwa na Madiwani, Waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wa dini (Wakristo na Waislamu) lilifanyika kwenye eneo la shule hiyo ya Lucky Vicent ambapo wakati wakiendelea kuzungumza wakiwa gorofani ghafla waliona Polisi wamefika kwa spidi na kusema watu wote wako chini ya ulinzi.

Baada ya hapo Polisi waliwakamata na kuondoka nao wote wakiwemo Waandishi wa habari wapatao kumi ambapo baada ya kufika kituo cha kati cha Polisi, Waandishi hao waliachiwa huru huku Polisi wakiwaambia hawana shughuli nao bali waliwapa lift tu kutoka kwenye eneo la tukio.

Kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika dakika chache baadae, Polisi walisema alieamuru Waandishi kuwekwa chini ya ulinzi na kupelekwa kituoni hakufahamu kwamba hao ni Waandishi na kwamba Wanahabari hao hawana kosa lolote na ndio maana waliachiwa muda mfupi baada ya kufika kituoni.

Kufuatia tukio hilo,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) imelaani tukio hilo.

"Tulikuwa tunahangaikia wenzetu waachiwe kwanza na hatimaye tumefanikiwa,wameachiwa huru bila masharti yoyote....maelezo ya kaimu RPC yanakera na kuchekesha,na kwa kweli ni kama kejeli....Eti waandishi hawakukamatwa bali walipewa 'lift' na Polisi kuwarudisha mjini wakati walienda na magari yao na yamebaki shuleni Lucky Vincent,ni jambo gumu kueleweka",ameeleza mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Claud Gwandu.

"Awali waliambiwa kuwa wamekamatwa kwa kukutwa kwenye mkusanyiko usio na kibali lakini waliokamatwa ni waandishi 9, meya wa Arusha,diwani mmoja na viongozi wawili wa dini..Hivyo basi,uongozi wa APC,pamoja na kulaani unyanyasaji huo wa wazi kwa .maelezo ya kina kuhusu kukamwaandishi wa habari,utaandika barua ya malalamiko kwa uongozi wa Polisi Mkoa kutaka atwa kwa wanahabari hao na baada ya hapo utachukua hatua stahiki",ameongeza Gwandu.

Katika hatua nyingine meya wa jiji la Arusha,madiwani,walimu,mmiliki wa shule ya lucky Vincent,viongozi wa dini waachiwa huru kwa dhamana kwa masharti kwamba watakapoitajika muda wowote wafike.

Inaelezwa kuwa wamepewa dhamana baada ya polisi kutaka hizo rambirambi zikabidhiwe kituoni hapo ili ufanyike utaratibu mwingine wa kuwafikishia walengwa jambo lililopingwa vikali na meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro.
Nikiwa Mtanzania, naitambua haki yangu ya kumtaka Rais wangu atende jambo fulani kwa faida ya Taifa langu.

Ninayo heshima kubwa kumtaka Rais wangu aache kuvitumia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika HALI YA KUNYANYASA WENGINE.

Namtaka afanye hivyo kwa sababu ninaamini kuwa HAIWEZEKANI HATA KIDOGO vyombo hivi muhimu kutumika ktk shughuli yoyote bila yeye kujua kwani nchi yetu haina AMIRI JESHI MKUU zaidi ya yeye.

Kutokana na ukweli huu, wananchi tunapata UHALALI wa kuamini kuwa ni yeye RAIS, akiwa Amiri Jeshi Mkuu, ndiye huamrisha haya kufanyika.

Tafadhali Ndugu Rais ninakutaka uhakikishe kuwa vyombo hivyo vinatumika kwa haki kwa maslahi ya Watanzania wote.
 
Mi ndo maana ya kibiti yananipa wakati mgumu maana kama wanamsifia aliyepiga risasi juu, hawamjui aliyetolea nape bastola, leo wanalazimisha lift....kweli kama raia mwema nitakuwa na uchungu na ya kibiti?nawaza...
 
Hivi wale waliopeleka wale watoto majeruhi marekani kutibiwa wamesha kamatwa ama?
 
Back
Top Bottom