Mwenye Masikio na asikie, Rais asiyetaka kuambiwa na amelaaniwa?

nndondo

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
1,251
895
Na mimi ni mmoja wa watanzania niliyesononeshwa sana na msiba wa vijana wadogo 33 kule Arusha, japo tunaambiwa kuwa idadi ni kubwa zaidi ya hiyo. Asubuhi hii tena ninaona tukio la vifo kule Tanga, kwenye ajali ya Coaster kugonga lori, tumeambiwa kuna vifo vya kutosha japo Idadi bado haijatangazwa. Tumepokea kwa moyo wote salamu za pole toka kwa Rais wa Kenya na tumeona wanachama wa Jubilee walivyo simama kwa dakika kuombea roho za marehemu

Huku kwetu kuna shida gani?
Katika vitu vyote kilichoniacha hoi ni kusikia Rais akimtumia salamu za pole Mkuu wa Mkoa, ana kwamba yeye haoni ukubwa wa hilo tatizo, ukisema atasema yeye yuko busy kutunyoosha na kutushikisha adabu, nimeona mch msigwa akijaribu kulizungumzia lakini kwa vile hatoki chama tawala, ameambulia matusi makubwa. Hivi jamani katika hali ya kawaida msiba huwa ni wa nani? si ni wa baba? kwa kawaida watu wote kwenye misiba watakua wanalia huku wakisubiri baba afike, huyu wetu nimesikia kamtuma Samia Suluhu kwa niaba yake yeye yuko busy, nachojiuliza mama Samia tumemzoe na tunampenda, tunaona kazi yake kubwa kitaifa ni kufungua mikutano, kana kwamba msiba huu utakaoshuhudia majeneza 33 kwa wakati mmoja hauna tofauti na mkutano wa kuazimisha siku ya kunyonyesha Tanzania.

Ni Misiba ama Kafara
Kwenye jamii zetu ambazo bado mila na mambo ya uchawi na kafara tuna masharti kwamba mhusika wa tukio hatakiwi kuhudhuria mazishi wala kuona maiti. Katika hali kama hii ya kiongozi wetu kupenda sana kuomba kuombewa tungetegemea maswala ya matukio ya kutisha yanayofanywa na mungu, akawa mbele akitafuta uso wa mungu badala ya kila siku kutaka atafutiwe uso huo, kwa mungu hakuna ku delegate hata kama wewe ni mkubwa. Sasa kutokuhudhuria janga hili la Msiba wa watoto hawa, kuna tuma ujumbe mbaya kwa sisi wengine, kwamba pengine labda hii ni sehemu ya mipango ya kutafuta nguvu za kiutawala.

Moyo Mgumu na kiburi ni machukizo kwa Mungu
Labda tu nimkumbushe mkulu ambaye anaonekana kuwa vizuri kiroho kuwa moyo mgumu ni machukizo kwa mungu. Tunaona wakati wa musa farao alipokuwa na moyo mgumu na mapigo aliyoyapata, Ndio maana najiuliza, je matukio haya ni Laana ya Mungu kwa Mkuu wa kaya? maana si jambo la kawaida kukutwa na majanga ya ajabu na yakutisha kama haya, tena yanayohusisha nguvu ambayo huna uwezo nayo, ni wakati wa mkuu kutafakari matendo yako ya uonevu na ubabe, kwa kuwa mungu anaona, Mwenye Masikio na Asikie maneno haya
 
Tukiachana na mengine ila huu msiba ni mkubwa sana kwa taifa letu, anyway Urais ni taasisi huenda wao wanajua kwa nini Mkuu wa nchi hajapangiwa kwenda huko.
Kwa sasa tuwape faraja wenzetu waliofiwa na wapendwa watoto wao, haya mengine tutendelee nayo huko baadaye
 
Tukiachana na mengine ila huu msiba ni mkubwa sana kwa taifa letu, anyway Urais ni taasisi huenda wao wanajua kwa nini Mkuu wa nchi hajapangiwa kwenda huko.
Kwa sasa tuwape faraja wenzetu waliofiwa na wapendwa watoto wao, haya mengine tutendelee nayo huko baadaye

Mlimchagua Wa nn
 
Hili tukio kwetu ni zaidi ya msiba. Maana tulipaswa tuomboleze hata siku tatu Kitaifa, Lakini huwezijua wengine wanavyolichukulia.
 
Back
Top Bottom