Mwenye kuifahamu hii company ya sdv notco limited 155

Mpendwa nikutahadharishe tu ukiombwa hela ya uniform jua unaenda kutapeliwa.
Ukishatoa hiyo hela usisahau kutupa mrejesho.
Habarini wadau. Natumai wote wazima.Msaada wa information tafadhali.
Kwa ambaye ana uzoefu na kampuni tajwa hapo juu naomba anitoe wasiwasi kidogo kwa kunifungua macho.

Nimeitwa kazini na hawa jamaa ila ninahisi dalili za upigaji kiaina. Nimejaribu kuwa-search kupata habari zao ila hamna maelezo ya kutosha.

Kabla sijapoteza muda wangu naombeni mwenye taarifa zake anijuze. Kwa madai yao wapo kurasini.
Asanteni. Siku njema.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Doooh!.. mbaya sana hii. Hata huyu kadai hela ya uniform.. Wala sitohangaika nao tena. Asantee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna kampuni kama Barrick Gold ,Geita Gold Mine na migodi mikubwa au taasisi nyingine wao kabla haujaanza kazi unafanya full body medical Check up wanalipia wao kampuni au kuna hospital zao.

Sasa mabaharia wa Buza wakitaka kukutapeli wanaweza kukuomba hela ya medical check up,hawa watu wapo very smart wanaweza kukodi mpk hotel watu wakaenda wakapigwa interview kwa hotel .

Mwisho wa siku unatumiwa SMS au unapigiwa ukaanze kazi ila wanataka hela ya medical check up kabla ya kuanza kazi ,wanaweza sema medical check up fee ni 100,000/=.

Ukitaka kujua utapeli utaona ukiwaambia sina hiyo hela wanaanza kunegotiate nawe,utasikia vipi hata 80,000/= hauna maana hii kazi mshahara 1.5M fanya hata ukope kesho uje kwenye medical wataendelea kukusumbua kwa SMS kukushawishi.

Ukifatilia kwa uliofanya nao interview kila MTU utakuta ameitwa kazini lakini story ni hile hile wazee wanataka mpunga wa medical check up.Wenye roho nyepesi wanalipa fasta fasta cha ajabu malipo ya kampuni kubwa ni kwa Tigo Pesa na sio bank.

Ukiona hivyo jua umekutana na watoto wa mbwa.
 
Juzi nilipost story ya dogo mmoja alivyotapeliwa huko huko Temeke,wajamaa wanaomba 60,000/= ya uniform .

Dogo alikuwa anauza biashara za kutembeza alikutana na mzee mmoja K/koo akamwambia kuna mchongo wa kazi kwa wiki 60,000/= unapata na ya chakula kwa siku 5000/= alipelekwa na mzee mmoja maeneo ya Temeke wakafika mpk ofisini mzee akaingia ofisini dogo akaambiwa asubiri nje kidogo ,mzee akajifanya anaenda kusuka mchongo na HR.

Baada ya dk 15 mzee akatoka akamwambia dogo unabahati kweli kweli kijana maana boss ndio nimemkuta ofisini kwake alikuwa anandaa orodha ya majina ya malipo si unajuha hii kampun ni mpya,kwa hiyo jina lako nishampa boss naye amekukubalia uanze kazi hata kesho.

Jamaa akamshukuru sana mzee,baada ya hapo mzee akamwambia dogo kwamba kesho inabd aanze kazi lakini kuna hela ya uniform kama 60,000/= inahitajika sababu bila Uniform hautoweza kuanza kazi.Dogo akasema hana kitu ana 30,000/= tu .Mzee akamwambia atamkopesha ili aongezee ila baada kufanya kazi wiki itabidi amlipe hiyo hela atakayomkopesha kuongezea hela ya uniform.

Dogo akasepa fasta fasta kweda kuvunja kibubu wakati huo yule mzee alikuwa anamsubiri kule Temeke alete ile 30,000/= aongezewe alipie uniform aanze kazi kesho yake .Dogo akarudi mpaka Jangwani alipopanga akavunja kibubu moja kwa moja akarudi Temeke kule alipomuacha mzee , kulipia hela ya uniform .

Mzee alipopewa hela akaingia ofisini akatokea mlango wa pili, dogo akasubiri masaa mawili bila mafanikio baadae akaanza kuisi ametapeliwa akaanza kulia kama mtoto mdogo anagaragara chini lakini hakupata msaada.

Ndio akanifuata kuniadithia kisa na mkasa kilichomkuta ili nimsaidie ikabidi ki ubinadamu nimtoe buku 5 ya kula,ili asogeze siku.

Kibaya zaidi kumbe ile hela aliyotoa dogo ilikuwa kodi ya nyumba,jioni mwenye nyumba (landlord) akaja kamtimua dogo sababu dogo alihaidi atalipa kodi ya chumba jioni baada ya kumsumbua landlord zaidi ya wiki 2,ofcorse alikuwa anaishi kwnye nyumba zile ambazo kodi unalipa mwa mwezi,au baba mwenye nyumba akiwa amekwama unampoza mnamalizana kwenye kodi.

Wahuni sio watu wazuri kabisa ,watafuta ajira wawe makini sana kipindi hiki cha mpito.
Dah ..Bro...Kuna dogo mmoja mitaa ya Temeke naye huwa analia na kujigaragaza akidai ametapeliwa ili apate huruma ya watu...au siyo huyo?

Sent using Beretta ARX 160
 
Phillip Petro HR Manager.
Naona hata linawezakua fake saabu nimecheki tigo pesa number anayotumia imesajiliwa jina la Evalista R

Sent using Jamii Forums mobile app

HR manager wa bollore ni mwanamke.. anaitwa Judith Nyafuru.. nimefanya kazi na hiyo kampuni miaka mitano japo nimeshasepa.. sio kampuni ya kongi longo ya kumuomba mfanyakazi hela ya uniform... nilikuwa warehouse department.. uniform kila mwaka mnapewa pea 2 mpya na safety boot... yaani kila mwaka lazima mpewe bureee..kila kitu bollore ni bure.. nakumbuka maziwa nilikuwa napewa makopo ya maziwa ya unga mpaka mengine napeleka nyumbani.. kabla halijaisha napewa lingine..

Ni kampuni nzuri sana ya kujifunzia kazi. Kama una taaluma ya logistics..

Zamani iliitwa Sdv notco, ikaja AMI ikaja SDV transami ikaja bollore.. majina yanabadilika badilika ila ni kampuni hiyo hiyo.. makao makuu ni tabata opposite kampuni ya magazeti ya mwananchi utaona makontena mengiii
 
Highly appreciated. Very detailed. Barikiwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kampuni kama Barrick Gold ,Geita Gold Mine na migodi mikubwa au taasisi nyingine wao kabla haujaanza kazi unafanya full body medical Check up wanalipia wao kampuni au kuna hospital zao.

Sasa mabaharia wa Buza wakitaka kukutapeli wanaweza kukuomba hela ya medical check up,hawa watu wapo very smart wanaweza kukodi mpk hotel watu wakaenda wakapigwa interview kwa hotel .

Mwisho wa siku unatumiwa SMS au unapigiwa ukaanze kazi ila wanataka hela ya medical check up kabla ya kuanza kazi ,wanaweza sema medical check up fee ni 100,000/=.

Ukitaka kujua utapeli utaona ukiwaambia sina hiyo hela wanaanza kunegotiate nawe,utasikia vipi hata 80,000/= hauna maana hii kazi mshahara 1.5M fanya hata ukope kesho uje kwenye medical wataendelea kukusumbua kwa SMS kukushawishi.

Ukifatilia kwa uliofanya nao interview kila MTU utakuta ameitwa kazini lakini story ni hile hile wazee wanataka mpunga wa medical check up.Wenye roho nyepesi wanalipa fasta fasta cha ajabu malipo ya kampuni kubwa ni kwa Tigo Pesa na sio bank.

Ukiona hivyo jua umekutana na watoto wa mbwa.
Doooh! .sante kwa kufungua macho watu tujueyanayoendelea. Sababu kazi ngumu tunakua desperate adi kuyumbishwa na wajinga wajinga hawa wapigaji. Sante sana kwa mchango wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom