Mwenye hekima na busara ni yupi

Mwenye hekima na busara ni yupi

Giro

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2009
Posts
359
Reaction score
24
Rais John Magufuli amemshangaa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwa kuidhinisha fedha za matibabu ya mpinzani wake wa kisiasa, Maalim Seif Sharif Hamad wakati alikataa kumpa mkono wa salamu walipokutana kwenye mazishi wiki mbili zilizopita.

“Mtu mmekutana kwenye msiba, mahali kwenye majonzi, mnamsindikiza marehemu. Kwa unyenyekevu wako Dk Dhein ukatoa mkono wako kumsalimia mtu fulani. Huyu mtu akakatalia mikono yake na bado asubuhi yake ukasaini fomu zake za kwenda kutibiwa nje ya nchi?” alisema Magufuli.

“Haya ni mapenzi makubwa sana. Amekataa mkono wako. Huyohuyo akiugua unampeleka hospitali. Akitaka kusafiri nje, unasaini na unampa na fedha na posho za kwenda nje. Mimi nisingeweza.”

“Niutoe mkono wangu, uukatae halafu kesho niende ofisini kukusainia wewe (akaongea kilugha). Ndiyo maana nasema wewe ni special. Nafikiri wanapotoka malaika wewe ndiyo unafuata. Kama mtu anaukataa mkono wako, na wewe kataa kufanya mambo yake, ajifunze kwamba na wewe mkono wako una thamani.”

“Mimi nilipata ushindi kwa asilimia 58, lakini hakuna mtu kutoka chama kingine atakayekanyaga mguu kwenye Serikali yangu.
"Mzee huyu ana moyo wa tofauti, namuomba Mungu apate hata robo ya moyo wangu maana amekuwa mpole mno,”
alisema Dk Magufuli.

“Mwenyeji anakuja na kuwaambia wageni wasije hapa na wao wamempuuza. Bado wageni wanakuja. Ukigombea mwaka wa kwanza ukashindwa, mwingine ukashindwa, mwingine ukashindwa, huwezi kujifunza hata kwenda kuuza nyanya sokoni kwamba biashara hii imekataa kwako,” alisema na kuongeza:

“Kwani hakuna wengine ambao wanakuja? Kuna mtu alitegemea kwamba nitakuwa Rais, hata kuota.Lakini nimekuwa waziri kwa miaka 20 sikujaribu hata siku moja kugombea (urais).

“Unajua vyeo hivi vinaletwa na Mungu, hata uzunguke namna gani, hata ufuge ndevu namna gani hata unyoe. Kama kasema hapana ni hapana tu, ndiyo maana nasema watu, ni shetani kama sivyo, basi ana moyo wa kishetani na mtu anayefarakanisha mke na mume kwa itikadi za vyama vyao pia ni shetani.

“Jana nilikwambia angalau uongeze kaukali kidogo. Umefanya mambo makubwa sana katika nchi hii. Tulishazungumza na wewe umezungumza kwamba kwa mujibu wa Katiba, uchaguzi umekwisha, ukisharudiwa umekwisha. Utarudiwa tena mwaka 2020, wazunguke waimbe lakini wewe ndiye rais,” alisema.

Rais ametoa kauli hizo akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani Unguja ambako amekwenda kushukuru wananchi kwa kumchagua kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.
 
Giro concluding remark yako ni ipi? ie take home message
 
hekima inaitaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!..................
 
Back
Top Bottom