Silasuga mahinyila
JF-Expert Member
- Dec 9, 2013
- 209
- 114
Wakuu,
kamwene,
Lengo la kuwaandikieni huu waraka ndugu zangu ni kitaka kuwaeleza fedheha kubwa inayoukabili mkoa wetu. Ninaombeni tujadili suala la wafanyakazi wa ndani na namna ya kuwasaidia.
Ndugu, Kwa miaka mingi sasa mkoa wetu umefanywa kuwa mgodi wa ma house girl. Wana wachimba watakavyo na kuwasafirisha watakavyo. wana wanunua kwa ahadi za uongo na fedha Ndugu, Wale mabinti ni ndugu zetu! Unaposoma natamani Kama Una damu na nyama basi chukulia kuwa huyu ni mwanao
Mjini maisha wanaishi magumu Mjini Chakula wanakula Kama wezi wanatengwa na wenye nyumba. Mjini Dada zetu wanatukanwa wanadharirishwa! Dada zetu hawapewi mishahara wengine! wanapigwa wanateswa kinyama na kufanyishwa kazi ngumu
Mjini asilimia kubwa wanawatumikia kingono mabosi zao na wanawao
wanajiuza pia ili wapate fedha ya kujisogeza . Hawana tumaini. Wengine kwa miaka mingi wamefungiwa hawajui nje wao ni ndani tuu. Ubinadamu haupo.Lakini sisi iringa hatujali tunaendelea kuwazaa na kuwauza hivi ni nani katuroga?
Hawa wanao pelekwa arabuni sitaki kusemea saana. maana mpaka wanakufa!
Lengo la waraka huu ni kwamba Ninania ya dhati ya kutengeneza sauti moja! Tuuambie ulimwengu kuwa sasa basi. Elimu bure watoto wetu wakasome Ifikie wakati tuwe na sauti moja kuwaaambia wana iringa kuwa mkoa wetu ni tajiri.. marufuku kuuza watoto! sio sifa sio utajiri kupeleka mtoto mjini akatumikie watu.
Ifike wakati! Tuwaambie waliopo mjini kuwa mnateseka! maana tusipo waambia wao hawajui Ifike wakati tuwe na chombo imara tuwaokoe waliopo kwenye mazingira magumu. Tuwaokoe , Tuwafundishe na tuwaendeleze...
Nitatoa mifano michache. Kuna mtoto wa kihehe Arusha alichomwa mikono, mtoto mdogo anamwaka tangu amalize darasa la Saba.
Yule aliye chomwa na pasi sehemu za siri maskini sijapata muda kumdadisi kuwa alitoka wapi lakini ndiyo naisha wanairinga wanaishi.
Ipo mifano mimgi ila naomba nimalise na mfano wa Dada X. Siku Nyumba ya bosi wake ilipigwa shoti Dada huyu alijitosa kukanyaga maji yaliyokuwa sakafuni.
Alipigwa shoti lakini maumivu hakuyasikia kwani alikuwa anataka kumuokoa mtoto wa bosi wake aliyekuwa ndani. Asingefanya hivyo yule mtoto asingalikuwa hai. Baada ya kutoka ndipo alipo gundua kuwa miguu haifanyi kazi . Alilazwa hospitali kwa miezi kadhaa. Leo miguu yake ni myeupe pee. Anakovu lisilo tazamika na kwakuwa amesha muokoa mtoto basi hawamuhitaji tena wamemrudisha kijijini . Hawezi hata kuolewa kutokana na majeraha mabaya.
Njoo tujadili namna ya kuwakomboa.
Aluta,~Continua