Mwenge: Ni Mwanga Tu Au Kuna Uvumba Fulani Unafukizwa Ili Kupumbaza Watanzania? Is it Justified?.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,

Hili ni swali tuu najiuliza kuhusu hizi mbio za Mwenge wa Uhuru zinazoendelea sasa. Kwenye Mwenge kinachokimbizwa nchi nzima, jee kweli ni ule mwanga tuu ili kumulikia na kuangazia, au ni ule moshi mzito mweusi kana kwamba kuna dawa fulani za uvumba zinazonyunyuziwa kama ubani, kisha zinatumika na Mwenge kuwafukiza Watanzania ili kuendelea kuwapumbaza ili waendelee....(naomba nisimalizie).

Rais Magufuli alipoingia tuu madarakani na kufuta maadhimisho ya sherehe muhimu kama ya Uhuru kwa hoja kuwa hazi justify the cost for spending so much kwenye sherehe tuu huku hospitali zetu zikikosa madawa na wagonjwa wanalala chini kwa ukosefu wa fedha. Moja kwa moja nilidhania kuwa sasa huu ndio utakuwa mwisho wa kuzungusha kwa Mwenge wa Uhuru. Lakini hali haikuwa hivyo.
Ingekuwa ni Amri Yake, Magufuli Angefutilia Mbali Mbio za Mwenge!, Jee Ni Amri ya Nani?!.

Hivyo hili ni swali kwa wenye ufahamu wa ndani kuhusu huu Mwenge, tuelezane ukweli jamani. Kinachozungushwa ni Mwenge lakini the essence ni ule mwanga tuu wa kumulikia au ni ule moshi unaofukizwa kama vile umetiwa mavumba fulani kuwapumbaza Watanzania?!.
.
Leo Mwenge umezungushwa wilaya yangu ya Kinondoni kupitia Barabara yangu ya Goba Rd. Askari wa kuzuia magari wametandazwa tangu mapema asubuhi. Askari hao hawana vifaa vya mawasiliano, zile radio calls za mawasiliano kujua msafara wa Mwenge umefika wapi, watu tumesimamishwa nusu saa nzima!.

Msafara ulipopita nilihesabu magari ya serikali tuu yalifika 50!. Does this kweli justify the cost time and resources kuzungusha Mwenge kumulika mchana? , au tunazungushiwa moshi ili kufukizwa kwa jina la Mwenge?!.

Nakumbuka nikiwa mwandishi wa habari kijana, nilipangiwa kuzunguka na Mwenge mkoa fulani, shughuli haswa ni pale mahali Mwenge unapolala, inakuwa ni mkesha wa Mwenge watu tunakesha usiku kucha, hakuna kulala.

Kinachofanyika katika shamrashara hizo za mkesha wa Mwenge ni hakuna kulala kweli, na kuna kwa baadhi ya watu utu unaondoka kabisa unageuka unyama!.

Kuna mambo ya faragha, mtu mzima mwenye akili zake timamu hawezi kuyafanya mahali pa wazi kwa kisingizio chochote kile, lakini kwenye mkesha wa Mwenge mambo hayo hufanyika hadharani tuu kwa kisingizio cha uwepo wa giza!. Na dada zetu nao sijui wanawehuka fulani, ukiita tuu wanakuja na ukigusa tuu unaitikiwa anajisongeza pembeni kwenye kigiza giza mnamalizana!. Kitu cha ajabu sio peke yenu bali kila kona ni vivyo hivyo, watu huku mnaonana watu wakimalizana!. Hiyo ndio shughuli kuu ya Mwenge wakati wa usiku kwenye mikesha ya enzi hizo, sijui sasa!.

Kazi ya kumulika huku wakifukiza ambayo hufanywa usiku mahali kwenye mkesha wa Mwenge, ni ziada tuu, maana shughuli muhimu ya Mwenge ni kuzindua miradi ya maendeleo mchana, sasa wakati wa usiku hakuna uzinduzi wa mradi wowote bali ni mkesha tuu na hayo yatokanayo.

Kufuatia shughuli hiyo kuu ya usiku ya shamra shamra za mkesha wa Mwenge ya hakuna kulala na ile hali ya ujana ni maji ya moto, nilitamani kila mbio za Mwenge nipangiwe mimi!.

Sasa hivi nimekuwa mtu mzima nikielekea uzeeni, sasa ndio natafakari na kujiuliza na hivi niliwezaje kuyafanya yale niliyoyafanya wakati wa ujana, ikiwemo yanayofanyika kwenye mikesha ya mbio za Mwenge, au tena mahali pa wazi na makundi ya watu kila mtu akiyafanya hayo hayo na mtu wake?!. Halafu ukimaliza na huyu uliyemalizana nao sio ndio unakuwa umetosheka, no! akitokea na mwingine anayevutia zaidi unajaribu tena na unakwenda tena pale pale ulipokwenda tena, kule mnapishana na yule mtu uliyeanza naye na yeye akiwa na mtu mwingine!. Sasa ndio najiuliza ilikuwaje au kwenye ule moshi wa Mwenge kuna mavumba fulani yananyunyuziwa kwa kufukizwa na ukinusa tuu huo moshi akili zinahama, unapumbazika na kujikuta unaweza kufanya lolote popote bila aibu?! .

Kwa wale ambao pombe zinawatuma vibaya mimi nikiwemo, mbona kila siku tunakunywa na tunalewa, na ukitokea unauhitaji wa huduma fulani utatafuta guest ya karibu kujihifadhi na kujipumzisha lakini kwenye mbio za Mwenge ni kutafuta kona tuu ya giza na makundi ya watu bila aibu yoyote?!, yaani binadamu tunakuwa kama wanyama!.

Kuna wanaodai mahali Mwenge unapolala huchaguliwa kwa makini, na kudai kuwa mahali hapo hufanyika matambiko fulani ya kimila, na kutolewa kafara!, japo mimi nimeshiriki kuripoti mbio za Mwenge na kulala kwenye mikesha ya Mwenge unapolala, sikuwahi kuona matambiko yoyote, wala kafara zozote zikitolewa, au kwa sababu giza likishaingia, mimi mawazo yangu yanahamia kwenye zile burudani za shamrashamra za mikesha ya usiku kucha hivyo kuwa bize na yale mengine hadi kutoona matambiko wala kafara!. Wenye ushahidi na hili zaidi ya huyu, Siri ya Mwenge wa Uhuru, jitokezeni mtuthibitishie.

Kama tuliweza kusitisha very important event ya maadhimisho ya Uhuru, alafu uki determine the cost, the time and the resources allocated kwenye mbio za Mwenge, lazima ujiulize kweli lengo la huu Mwenge ni mwanga tuu wa kumulika au pia ni ule moshi, ndani yake kuna kitu kingine muhimu nyuma yake?!.

Mafuta Ya Mwenge na Sumu ya Cabon
.
Wakemia huu Mwenge unatumia mafuta gani yenye moshi mweusi mzito hivyo?. Kwa msio jua moshi mweusi ni sumu ya cabon ukivutwa sana husababisha magonjwa ya TB, Bronchitis na Cancer. Jee kuliwahi kufanyika utafiti hao wakimbiza Mwenge hua wanaishi muda gani humu duniani baada ya mbio za Mwenge?.

Kama lengo la Mwenge ni ule mwanga ili umulike, ulipoanzishwa ile 1961 kwa mafuta yale, hiyo ndio ilikuwa technology ya wakati huo, leo miaka 50 baadae kuna technology kibao za kuzalisha mwanga tena mkali zaidi ya huo wa mafuta yenye sumu, kwa nini tuendelee kuwauwa Watanzania wenzetu kwa sumu huku kuna lots of alternatives ambazo hazina sumu.

Hivi tungetumia source ya gesi badala ya mafuta ya Mwenge na tungesave kiasi gani?.

Badala ya kutumia hayo mafuta mazito yenye sumu kibao ya carbon, kwa nini tusingetumia methene ambayo ina mwanga na haitoi moshi?, au pia maelekezo ya mafuta hayo ya Mwenge pia ni maelekezo ya mganga wa Mwenge na hakuwahi kuulizwa kama tunaweza kuyabadili?.

Vijana wa UVCCM mliyemo humu, njooni na idadi ya wakimbiza Mwenge toka Uhuru, mtueleze wangapi wako hai hadi leo. Na kama kuna waliotangulia mbele ya haki ni wangapi, sababu za vifo vyao na kama ni maradhi ni maradhi gani na yaliwapata muda gani tangu baada ya mbio za Mwenge?.

Hata hivyo sitashanga kama watatokea watetezi wa kujustify this lavish spending and time wasting kama ilivyotokea mjadala wa umuhimu wa wakuu wa wilaya, ma DC ambao Katiba ya Warioba iliwafutilia mbali na kazi zao kufanywa na Wakurugenzi wa Halmashauri.
Kama Tanzania tunataka maendeleo ya kweli ni lazima tuwe very serious kwa kuachana na kuendekeza matukio stereotype na kumaitains positions ambazo ni redundancies just to maintain a status quo, kwa vile zilikuwepo! .

When are we gonna change? . Yaani kwa Magufuli huyu aliyefuta sherehe za Uhuru lakini ana maintain mbio za Mwenge, huu Mwenge una nini haswa? . Tuelimishane jamani!.
Jumatano njema.
Paskali
update.
Forojo Ganze (Master), mchawi maarufu aliyeanzisha Mwenge wa Uhuru
 
Hivi ungewekwa tu pale Makumbusho tukaupelekea kapipe ka gas ukawa unawaka tu mwaka, miaka mpaka karne kuna shida gani? na hizi gharama zikaenda kufanya kazi kwingine...

Gharama za kuukimbiza vs Faida yake kwa taifa, halafu eti kuna mtu anasema tunabana matumizi...
 
Kaka Pascal mimi nakumbuka ulikesha kijijini kwetu Ngonga nilikuwa primary darasa la tano,kutokana na kuwa na ufahamu kidogo kila kona nilikuwa naona watu wamelaliana sasa nikawa sielewi. Kesho shuleni tukaambiwa tuandike insha kuhusu mwenge kutokana na utoto nilichoandika acha walimu wacheke mpaka machozi yaliwatoka,mwenge haufai.
 
Mwenye akili angekuja na Idadi na thamani ya miradi iliyofunguliwa na Mwenge toka tupate uhuru VS Gharama zilizotumiwa na Mwenge.

Hii ndio njia ya kisayansi ya kuujadili mwenge !!
Duh, yaani unaakili za ajabu Sana jingalao , unatetea kila kitu, ngoja nikuulize, kwa mfano hiyo miradi ingezinduliwa Tu na mwenyekiti Wa mtaa eneo husika ingeathiri vipi hiyo miradi katika utendaji/uzalishaji wake?

Vipi gharama za kukimbiza mwenge nchi nzima zingejenga viwanda vingapi? Inakuaje Sherehe za Uhuru Ni haramu ILA sherehe za Mwenge Ni halali? Ni sawa na kusema hulikitimoto ila mchuzi wake unakunywa!!!

Watanzania sio wajinga kiasi hicho.
 
Mwenye akili angekuja na Idadi na thamani ya miradi iliyofunguliwa na Mwenge toka tupate uhuru VS Gharama zilizotumiwa na Mwenge.

Hii ndio njia ya kisayansi ya kuujadili mwenge !!

Unataka kusema kuna uhusiano wa ujenzi wa miradi ya maendeleo na mwenge? Je hakuna njia nyingine nzuri na rahisi za kuzindua miradi ya maendeleo?

Je fedha za mwenge (makato ya lazima kwa watumishi wa umma, michango ya lazima na hiari, kodi za wananchi nk) kweli zinahalalisha zinaa, wizi, vifo, unyang'anyi na machafu mengine yanayotokea kwenye mikesha na misafara ya mwenge?

Unajua hizo mbio huambatana na vifo/ajali nyingi tu? Unajua kweli historia ya mwenge wewe? Ni viongozi wangapi wa mbio za mwenge waliokufa muda mfupi baada ya kilele cha mbio au waliopatikana na maswahibu?
 
Paskali;
Mimi si mganga wa kienyeji wala sina uganga/uchawi lakini nataka kukuunga mkono katika matamshi ulo tamka kuwa huenda kuna uvumba flani huwekwa ndani yake kuwapumbaza watz.
Hicho kinachowafanya wakuu wasione hiyo gharama ya kulilinda "bati" hilo kwa mbwe mbwe zoote. Lipigiwe ngoma za kienyeji usiku kucha, watoto wasio na baba wazaliwe/watungwe mimba sio chini ya 100 kila siku usiku mahali flani. Serekali isione hiyo hasara na hatari kwa taifa. Nasema hawataki kutuambia ila kuna jambo nyuma ya pazia. Uasherati unaofanyikaga kila mwenge unapokesha sio siriiiii. Magonjwa yanayoachwa hapo kijijini si ya kawaida. Iweje serekali iyapuuze iuone mwenge kuzimika ni hasara kuliko madhara yanayoletelezwa nao??
 
Back
Top Bottom