Mwenendo mbaya wa Matokeo ya Simba SC. Je, nini kifanyike kuinusuru irudi kwenye makali yake?

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,238
Salaam Wakuu,

Hawa Jamaa zetu kipi kimewatokea? au hawajazoea kukaa kileleni? ni nini hasa kinachowakabili? au ndio mishahara ya Mwezi wa 12 haijaingia mpaka saa hizi?...

Wenye timu yenu mje mtuambie! Hivi Kichuya mlimpeleka wapi kwa mkopo? mbona haonekani siku hizi?

Hivi kweli nyinyi mnataka ubingwa au mnamtisha tu Yanga kuwa nanyi mnaweza kuwa Mabingwa?

Najiuliza haya yote kwa kuwa sielewi elewi! Maana tangu mtoke zenji ambako nako mlisema mtakuwa Mabingwa, mmekuwa Matasa kabisa. Yaani sijui mmegoma kufunga au ndio mgomo wa chinichini? Ni kitu gani mnataka Mo Dewji awafanyie ili mrudi kwenye ubora wenu?

Kama mnamuogopa MO Dewji mtumeni Mgosi aende kwa Manji, huena atapata msaada wa chochote kitu ambacho kitawapa morali.

Hivi vya nguruwe sio vizuri kabisa....ndio hivi huwafanya wanafunzi washindwe kuendelea na Masomo. Mara jana Ka'moja na leo Ka'moja....mara kesho hupokei ka'moja na wala hutoi hata hako Ka'moja...!

Kunani huko? Sisi haoooooooooo tunajongea palipo petu(yaani pale juu)..... hiku nikikuacha ukisumbuka na Viwanja vya Manundu manundu...!

Ila hakikisha huchezi kwa pressure mno ...maana ukitumia pressure mno nina uhakika akina Ajibu na Mkude wakavaa jezi ya Njano na Kijani msimu ujao pale Jangwani!

Kila la kheri mtani! Lipia kisimbuzi chako mapema...maana akina Niyonzima wanavyopena sifa ...sijui wamekuandalia nini hapo Kesho wakutanapo na Mwadui kwenye 'Kapeti' la Taifa pale.

Ni mimi...

DemiGod.
 
Kamuulize omog na Aveva
Aisee! kwa hivyo wao ndio wana majibu......

Maana Mashabiki wao wako kwenye hali mbaya kweli....

Mimi ningekuwa shabiki wa Simba ningewaita mashabiki wenzangu wote na kuanza kuandamana tukielekea Ofisini kwa Aveva na Nyumbani kwa Omog...
 
Kwisha habari yao,pumzi imekata wamechoka nyang'anyang'a kifo cha mende,chalii.
Nawaonea huruma mno...

unajua kuwa viongozi wa hii klabu huwalaghai mashabiki wao kila msimu kuwa watakuwa mabingwa...alafu wakikosa ubingwa wanageuzia lawana hizo kwenda kwa Manji,Marefa,Linesmen,Viongozi wa ngazi za juu wa TFF na Mashabiki wote wa Yanga SC kuwa ndio sababu ya klabu yao imekosa ubingwa!
 
Nafikiri hilo swali ni zuri japo ni la kinafki.Ila lielekeze kwa wafuatao
1.Malinzi na TFF
2.Omog
3.wala rushwa wote wa mpira wa Tanzania.
3.Aveva kwa usajili wake wa kipuuzi wakusajili viungo tu bila stricker.
SIMBA WAMEFUNGWA KWA UZEMBE WAO WENYEWE.
 
Hakuna sababu ya kuwalaumu Simba kwa kufungwa na Azam leo kwa sababu Uwezo wa Azam kimpira kwa sasa uko juu sana, Azam kwa sasa wako kwenye Peak ya uchezaji wao, hata warudiane mara 10 bado simba atapokea kichapo tu. Na sio Simba tu, hata Yanga pia.

Kiufundi, Azam ndio timu bora zaidi hapa Tanzania. Kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, wameonyesha mabadiliko ya hali ya juu.
 
Mkuu

si wamesajili ma striker 4 msimu huu

1.Mavugo (Mkata mabeki)
2.Athanas (kwa sababu amemfunga Yanga)
3.Blagnon (Mkata upepo)
4. Luizio (Mkata walinzi)

......
 
Kiufundi, Azam ndio timu bora zaidi hapa Tanzania. Kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, wameonyesha mabadiliko ya hali ya juu.

Mkuu hata pia walipo toa sare na Mbeya City bado utawaweka kama ndio klabu bora zaidi hapa bongo?

Aha utani mkuu...unanichekesha mno aisee!
 
mashabiki wa mpira wa tz noma sana simba kafungwa mechi ngapi? tuanzie kwanza hapo.
 
Hakuna sababu ya kuwalaumu Simba kwa kufungwa na Azam leo kwa sababu Uwezo wa Azam kimpira kwa sasa uko juu sana, Azam kwa sasa wako kwenye Peak ya uchezaji wao, hata warudiane mara 10 bado simba atapokea kichapo tu. Na sio Simba tu, hata Yanga pia.

Najua kuwa sio kosa lako!

Kusema ''hata Yanga pia.''! lakini ni kweli hujakosea. Azam akirudiana hata mara 10 na yanga, ni lazima Yanga atafungwa.

Ila kati ya hiyo mara 10. kama kutakuwa na mechi unayohusisha kuwania ubingwa...huenda yakasemekana mengine..

Mentality ya klabu yetu huwa iko hivi......kutufunga utatufunga ila ni kwenye mashindano ya kipuuzi tu...Kama vile Mtani Jembe, Mapinduzi, nk...

ila kutufunga kwenye mashindano ambayo yanagusa mafanikio ya Klabu, hapo labda ukachinje kuku katikati ya bahari ya hindi.
 
mashabiki wa mpira wa tz noma sana simba kafungwa mechi ngapi? tuanzie kwanza hapo.
sio kufungwa mechi ngapi..

swala ni jinsi unavyo ''surrender'' usukani ukiangalia nyuma unamuona jamaa anazidi kukupumulia mgongoni..

kuna pressuer sana mahala pale kama hujapazoea lazima upaachie...

ila jambo zuri kutoka kweni ni kuona jinsi mnavofanya effort ya kutaka kupazoea maha pale....ili baaa ya misimu michache angalau mkaepo mpaka mwisho wa msimu..
 
Wawatumie under 20 wao wana upepo wa mataji

Sikuhizi walisha achana na ile philosophia yao ya kujigamba kuwa wao ndio klabu pekee TZ kulea na kukuza wachezaji...

Baada ya kuona Yanga SC akiendelea kuokota makombe yake ya ligikuu wakaoo hapana isiwe tabu ngoja tuachane na kukuza akina ndemla ....kwa sababu hata trukikuza bado wataenda kujiunga na Yanga SC.........
 
Salaam Wakuu,

Hawa Jamaa zetu kipi kimewatokea? au hawajazoea kukaa kileleni? ni nini hasa kinachowakabili? au ndio mishahara ya Mwezi wa 12 haijaingia mpaka saa hizi?...

Wenye timu yenu mje mtuambie! Hivi Kichuya mlimpeleka wapi kwa mkopo? mbona haonekani siku hizi?

Hivi kweli nyinyi mnataka ubingwa au mnamtisha tu Yanga kuwa nanyi mnaweza kuwa Mabingwa?

Najiuliza haya yote kwa kuwa sielewi elewi! Maana tangu mtoke zenji ambako nako mlisema mtakuwa Mabingwa, mmekuwa Matasa kabisa. Yaani sijui mmegoma kufunga au ndio mgomo wa chinichini? Ni kitu gani mnataka Mo Dewji awafanyie ili mrudi kwenye ubora wenu?

Kama mnamuogopa MO Dewji mtumeni Mgosi aende kwa Manji, huena atapata msaada wa chochote kitu ambacho kitawapa morali.

Hivi vya nguruwe sio vizuri kabisa....ndio hivi huwafanya wanafunzi washindwe kuendelea na Masomo. Mara jana Ka'moja na leo Ka'moja....mara kesho hupokei ka'moja na wala hutoi hata hako Ka'moja...!

Kunani huko? Sisi haoooooooooo tunajongea palipo petu(yaani pale juu)..... hiku nikikuacha ukisumbuka na Viwanja vya Manundu manundu...!

Ila hakikisha huchezi kwa pressure mno ...maana ukitumia pressure mno nina uhakika akina Ajibu na Mkude wakavaa jezi ya Njano na Kijani msimu ujao pale Jangwani!

Kila la kheri mtani! Lipia kisimbuzi chako mapema...maana akina Niyonzima wanavyopena sifa ...sijui wamekuandalia nini hapo Kesho wakutanapo na Mwadui kwenye 'Kapeti' la Taifa pale.

Ni mimi...

DemiGod.
Hatushauriwi wala hatupewi miongozo au nini cha kufanya na watu wanafiki kama wewe..

Hivo yaani.
 
Nafikiri hilo swali ni zuri japo ni la kinafki.Ila lielekeze kwa wafuatao
1.Malinzi na TFF
2.Omog
3.wala rushwa wote wa mpira wa Tanzania.
3.Aveva kwa usajili wake wa kipuuzi wakusajili viungo tu bila stricker.
SIMBA WAMEFUNGWA KWA UZEMBE WAO WENYEWE.

Hii orodha inanichekeshaga sana...

Ndiyo ambayo hutumiwa sana na viongozi wa juu wa simba pale wakosapo Ubingwa wa VPL ili kukwepa lawama za mashabiki wao .

1. TFF
2. Malinzi
3. waamuzi
4. Manji
5. Viwanja
6. Kocha wao!

hahahahahahahah
 
Back
Top Bottom