Gwappo Mwakatobe
R I P
- Nov 22, 2019
- 1,796
- 2,345
Kuna bango humu JF lisemalo "Mfumo wetu wa Muungano ni janga la Kitaifa"Danadana za kupata KATIBA MPYA NA BORA zinaendelea, na kuendelea kutafuna fedha za umma kwa mabilioni.
Maoni ya Nyalali yalitupwa, Kisanga alifokewa na Mkapa, Warioba akashambuliwa na Kikwete na hadi kupigwa ngwala na kijana wake Makonda ambaye alipewa zawadi ya ukuu wa wilaya ya Kinondoni.
Aliyepo alikuja na Kikosi Kazi cha kupata KATIBA MPYA na mwishowe akasema maoni ya Kikosi Kazi si amri. Hivi majuzi Machi 8 kasema ataunda kamati ya KATIBA MPYA. Danadana zinaendelea!
Nyalali: Season 1
Kisanga: Season 2
Warioba: Season 3
Bunge la Katiba na Katiba Inayopendekezwa: Season 4
Mukandala na Kikosi Kazi: Season 5
Kamati ya KATIBA MPYA: Season 6
Nanihii (!?): Season 7
...tunasuburi. Mwishowe yote yatatupwa na kuendelea na seasons!
Ili tuje kupata KATIBA MPYA NA BORA tunahitaji chama mbadala, serikali mbadala na viongozi mbadala. CCM na upinzani uliopo tupa kule! Huo utakuwa ndio mwisho wa danadana na seasons zake.
Naam!Naunga mkono hoja kwa 💯%
Watanzania tunahitaji Katiba ya Wananchi! Na siyo Katiba kwa ajili ya kuinufaisha CCM, au Chadema.
Tunahitaji Katiba ya kuinufaisha nchi na wananchi wake wote! Na siyo kikundi cha watu wachache, mfano wanasiasa, nk.
Inauma sana!Kuna bango humu JF lisemalo "Mfumo wetu wa Muungano ni janga la Kitaifa"
Kwa mfumo huo Hauruhusu kuanzisha mchakato wa katiba mpya.
CCM wenyewe wame kwama hawajui waanzie wapi , na hawaju walipo kwama.
Nyerer Na Mzee karume wametuingiza Chakani.
Nchi inaangamia kwa Ufisadi, pesa zinaliwa kurekebisha hili na lile , kamati na makongamano yanaua mamilioni
Mgosi hiyo katiba ya kunufaisha watu wote, kwa Africa ni vigumu kupatikana,Naunga mkono hoja kwa [emoji817]%
Watanzania tunahitaji Katiba ya Wananchi! Na siyo Katiba kwa ajili ya kuinufaisha CCM, au Chadema.
Tunahitaji Katiba ya kuinufaisha nchi na wananchi wake wote! Na siyo kikundi cha watu wachache, mfano wanasiasa, nk.
Ni kweli kabisa mghoshi (mgosi), tuna mafisadi na walafi wa kutisha na kulitesa taifa. Tuombe Mungu aingilie kati na kutunusuru.Mgosi hiyo katiba ya kunufaisha watu wote, kwa Africa ni vigumu kupatikana,
Viongozi ni wabinafsi sana, wanatembelea magari ya milion 600, walipa kodi wanakunywa maji ya tope na mifugo,
Kila mmoja anatamani kupata nafasi ili akaibe na kujinufaisha yeye na familia, ukoo wake na marafiki zake,
Nchi imekuwa kila kiongozi hupandikiza mwanae au ndugu ili akistaafu, aendelee kuneemeka na jasho la wanyonge,
Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
Shukrani sana!Tafadhali tembel
https://www.jamiiforums.com/threads/mfumo-wa-muungano-ni-janga-la-kitaifa.2069546/ea bango hilo uone kuwa suala la Katiba ni Majanga
Mwisho wa siku yote yana mwisho hapa chini ya jua.Kuna vitu wanaamini vitakuwa vikwazo kwao, utafikiri wataishi milele
Mali na watoto ni Fitna
Na wengi wanaangukia hapo
Ukweli mchungu. Inabidi tuwe kama na kipindi kifupi cha mpito ambacho hatutakuwa chini ya uongozi wa hawa wanasiasa uchwara.CCM na upinzani uliopo tupa kule! Huo utakuwa ndio mwisho wa danadana na seasons zake.
Uko sahihi kabisa na hayo ndiyo mabadiliko sahihi!Ukweli mchungu. Inabidi tuwe kama na kipindi kifupi cha mpito ambacho hatutakuwa chini ya uongozi wa hawa wanasiasa uchwara.
Kweli mkuuMwisho wa siku yote yana mwisho hapa chini ya jua.
Issue isiwe kupatikana katiba tu, hiyo katiba itakuwa na ubora gani ndio swala la muhimu.Majira ya kupatikana KATIBA mpya Tanzania yamefika.
Tutakamilisha kupatikana kwa Katiba mpya 2026,
KATIBA Bora itadaiwa Kwa maandamano,Issue isiwe kupatikana katiba tu, hiyo katiba itakuwa na ubora gani ndio swala la muhimu.
Mfumo wa muungano wetu ni moja ya mambo yanayokera, lakini ccm hawako tayari kubadilika kwenye hili. Tunafanyaje?!
Upo tayari kuandamana?!KATIBA Bora itadaiwa Kwa maandamano,
Haiji Kwa kuridhiana mezani Kwa vyama vya siasa.
Get ready.