Mwendawazinu awakimbiza watu ovyo crdb

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Mwendawazimu akimbiza watu Benki

5868834.jpg

Friday, August 05, 2011 12:26 PM
WAFANYAKAZI wakiwemo wateja waliofika jana Benki ya CRDB, tawi la Azikiwe walijikuta wakikimbia huku wengine wakianguka kwa presha kufutia kijana mmoja aliyekadiriwa kuwa na upungufu wa akili kurusha mawe kwenye vioo vya benki hiyo.
Majira ya mchana jana tukio hilo lilitokea na kusababisha wafanyakazi na wateja waliokuwemo ndani ya benki hiyo kuanza kukimbia ovyo wakidhani wamevamiwa na majambazi.

Huku baadhi ya wafanyakazi wakiacha majukumu yao na kulala chini huku wengine wakikimbia ovyo kwa kunusuru maisha yao bila kujua kilichokuwa kikijiri nje

Hali hiyo ilifanya askari polisi kufyatua risasi hewani, ili kuzuia uharifu zaidi na ndipo kijana huyo alipoonekana akiwa katikati ya Barabara ya Azikiwe na Maktaba eneo la Posta Mpya akiendelea kurusha mawe kwenye vioo hivyo

Ndipo kijana huyo alipokamatwa na kutiwa mbaroni japo alionekana si mwenye akili timamu huku baadhi ya watu wakidai kijana huyo ni mwendawazimu huku wengine wakidai ameathirika kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya

Kufuattia hali hiyo baadhi yawateja walizirai kwa hofu na wengine wakionekana wakilia kutokana na kupotelewa na nyaraka zao muhimu, fedha wakiwa ndani ya benki hiyo zikiwemo kadi na fedha taslimu.

NIFAHAMISHE ilibahatika kuona mwanamke mmoja aliyekuwa ameanguka chini kwa hofu na hali yake iloikuwa tata kutokana na hali hiyo
 
Pale CRDB azikiwe kuna mgambo mmoja ambaye namwonaga sana pale na anakua active sana imekuaje ameshindwa kumdhibiti,halafu jamaa wa security wameshindwa kutoa taarifa kamili kwa wateja wao ni nini kinachoendelea ili watulie?
 
Back
Top Bottom