Mwenda: TRA sio kodi tu bali kulinda usalama mipakani

Mwenda: TRA sio kodi tu bali kulinda usalama mipakani

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusufu Mwenda, amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha usalama wa nchi na raia wake kupitia udhibiti mkali wa bidhaa zinazoingia mipakani.

Soma pia: Sasa turudi kuijenga nchi TRA iwe jeshi usu, hakuna mwananchi wa kukwepa kulipa kodi

Akizungumza Januari 25, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Bonanza la kuelekea Siku ya Forodha Duniani 2026, Kamishna Mwenda amesisitiza kuwa maafisa wa TRA wanafanya ukaguzi wa kina kwa kila kitu kinachoingia nchini ili kuzuia bidhaa haramu na zinazoweza kuleta madhara.

Mwenda amebainisha kuwa, ingawa TRA inafahamika zaidi kwa kukusanya mapato yanayochochea maendeleo ya nchi, jukumu lake la ulinzi wa jamii ni la kipaumbele cha juu. Amesema usalama na amani vilivyopo nchini kwa sasa vinatokana na weledi wa maafisa forodha katika kuzuia vitu visivyoruhusiwa, ikiwemo bidhaa zinazoweza kuhatarisha afya za wananchi na mazingira kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom