MWANZA: Watoto wanne wateketea kwa moto

MWANZA: Watoto wanne wateketea kwa moto

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,606
Watoto wanne wa familia moja wamefariki dunia kwa kuteketea kwa moto walipokuwa wamelala chumbani katika tukio lililotokea mtaa wa Geita Road Kata ya Nyatukala mjini Sengerema.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole amesema tukio hilo lilitokea saa tano usiku wa Februari 28, 2018 na kuwataja watoto hao kuwa ni Redia Elias (10), Modesta Elias (9), Steven Deogratias (9), na Kizengela Elias mwenye umri wa miaka ninane.

Amesema wakati moto huo uliotokana na mshumaa kushika chandarua na kuunguza godoro walilokuwa wamelalia, mama yao alikuwa amelala kwenye nyumba nyingine ya familia hiyo.

“Watoto wote ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Pambalu na wanatarajiwa kuzikwa kesho,” amesema Kipole.

Mmoja wa majirani wa familia hiyo, Amas Juma amewataka wazazi kuwa makini pale wanapolazimika kuwawashia watoto mishumaa kwa kuhakikisha inazimwa kabla ya kulala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuchukua tahadhari watoto wanapobaki wenyewe nyumbani.


Mwananchi
 
Chanzo kimeonekana ni mshumaa kushika chandarua then godoro uchunguzi mwingine upi tena. Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema watoto amen
 
Ohh no vimalaika jamani!
Rip
 
Chanzo kimeonekana ni mshumaa kushika chandarua then godoro uchunguzi mwingine upi tena. Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema watoto amen
Me mwanyewe nashangaaga hawa police wa shithole countries uchunguzi gani wakati chanzo cha moto ni candle
 
Hatari sana na inakuaje mpaka moto unakua mkubwa wazazi wanakua na usingizi gani huo wa porno nn hata kusikia harufu ya moshi tu hamna na je kama ni getho la nje inakuaje watoto walale peke yao huu ni uzembe wa mwendokasi
 
Nani anatumia mshumaa wakati sola zimeenea nchi nzima? Yaani anaenda kulala kwa jirani unaacha watoto, aseme ukweli, au alienda kuchepuka huku nyuma watoto wakatiwa kiberiti? nawaza tu kwa sauti!
 
Wamkamate huyo bwana aliyekuwa nae na mke wa huyo hawara jibu litapatikana, msijesema huyo nae ni chadema.
 
Chanzo kimeonekana ni mshumaa kushika chandarua then godoro uchunguzi mwingine upi tena. Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema watoto amen
Kuna mengi ya kuchunguza hapo kumbuka mama wa watoto ati alilala nyumba nyingine, kivipi? Je umeme ulikatika wakawasha mshumaa au nyumba haina umeme hadi kupelekea kutumia mshumaa, sababu zilizomfanya mama aache watoto na kwenda kulala huko, hadi watoto wanatekea kabisa majirani walikuwa wapi ina maana watoto hawakupiga kelele? tuache uchunguzi ufanyike

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Oh, INASIKITISHA SANA WAPUMZKE KWA AMANI. WANAKUFA WATOTO WEMA WANABAK WATU WENYE ROHO MBAYA.
 
Muwe na makazi mema huko muendako.. Tupo nyuma yenu.
Kifo jamani kifo duuh!! Laleni salama watoto katika usingizi wa milele
 
Chanzo kimeonekana ni mshumaa kushika chandarua then godoro uchunguzi mwingine upi tena. Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema watoto amen
Hawa watu wanapenda sana kukimbilia kusema mambo ya uchunguzi....
 
Me mwanyewe nashangaaga hawa police wa shithole countries uchunguzi gani wakati chanzo cha moto ni candle
Inawezekana ni negligence ya wazazi, au au wazazi walikuwa na motive, au ni bahati mbaya tu....yote yanawezekana.
 
Basi hapo wapinzani watasema wameuliwa na CCM, ngoja tusikie Mbowe ataropokaje hapa.
 
Back
Top Bottom