Mwanza: Wanaume wa kata ya Mabuki wilayani Misungwi, wapaza sauti kilio chao cha kunyimwa unyumba

Drizzy2

Senior Member
Jun 8, 2012
152
105
Wanaume wa mikoani hii nini sasa mnatutia haibu bora sisi wa dah....! Picha inajieleza

Wanaume katika kata ya Mabuki wilayani Misungwi mkoani Mwanza wameiomba Serikali kuingilia na kusikiliza kilio chao cha kunyimwa unyumba na wenza wao (wanawake) kwenye ndoa kutokana na tatizo hilo kuzidi kuwa kubwa.

=====

Baadhi ya wanaume katika Kijiji cha Mwanangwa Kata ya Mabuki wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza, wamedai mifarakano baina ya wanandoa, usaliti na umaskini wilayani humo inatokana na wanawake kuuza mavuno ya mazao kinyemela ili kununua vipodozi.

Madai hayo yamekuja siku chache baada ya wanawake kudai kutelekezwa na waume zao nyakati za mavuno kutokana na kuchukua fedha za mauzo ya mazao mbalimbali kisha kwenda kutumia na wanawake wanaofanya ukahaba kutoka Jijini Mwanza ambao wamepewa jina la ‘Nzige’.

Wakizungumza juzi kwenye mdahalo maalumu wa kujadili namna ambavyo kipindi cha mavuno kinakuwa na changamoto wilayani humo, ulioandaliwa na Shirika la Kutetea haki za Wanawake na Watoto la Kivulini, wamesema migogoro mingi huzuka wakati wa mavuno.

Mmoja wa wanaume waliochangia kwenye mdahalo huo, Mussa Kiyumbi, amesema chanzo cha migogoro na hata kupigwa kwa wanawake katika ndoa, kimekuwa kikitokana na wao kuwanyima unyumba lakini pia huuza mazao kinyemela ya familia kinyemela.

“Wanawake hawa wanauza mazao kinyemela kwa lengo la kwenda kununua vipodozi ambavyo waume zao hawavijui, wanabeba mazao kidogo kidogo kwenye ndoo na kwenda kisimani kama wanaofuata maji, changamoto nyingine tukidai haki zetu za ndoa wake zetu hawaridhii ndiyo maana tunatoka nje kutafuta suluhu na kupoza hasira kwa Nzige,” amesema.

Mmoja wa wanawake wilayani hapo, Regina Kubunga, amesema wanawake wengi wamekuwa wakiamua kuuza mavuno ya mazao ya akiba kwenye nyumba zao ili kumudu gharama mbalimbali kutokana na wanaume kuuza na kumalizia fedha zote kwenye anasa na ulevi.

“Unakuta nyumbani hamna hata bustani ya mboga, hufugi kuku sasa wanapokuja wageni baba hayupo, inabidi uhangaike hayo ndiyo matokeo yake wanawake nao huchukua kwenda kuuza sehemu ya mazao ili wapate fedha za kutatulia matatizo, hivyo sababu ni wanaume kushindwa kutimiza wajibu wao wa kutunza familia,” amesema.

Chanzo: Mtanzania
 

Attachments

  • Screenshot_20180712-111003.jpg
    Screenshot_20180712-111003.jpg
    72 KB · Views: 70
Hii News niliisikia kwenye magazeti, haikuingia akilini wananyimwa vipi wakati wako kwenye ndoa, labda aliyefanikiwa kuipitia hiyo taarifa atufafanulie.
 
we unafkiri mchezo mziki si mdogo lazima waombe poo...yani ukiingia nyumbani mke inabidi anune akikumbuka kichapo cha jana yake anatamani arudishe mahari
 
we unafkiri mchezo mziki si mdogo lazima waombe poo...yani ukiingia nyumbani mke inabidi anune akikumbuka kichapo cha jana yake anatamani arudishe mahari
Sasa akikumbuka kichapo ndio akunyime hadi mkalalamike tena mnaiomba selikari iwasaidie kuwaombea mpewe mnatia haibu mikoani
 
Siku zote ninasema wavulana wa mikoni hamna kitu, na bado watoto wanaozaliwa kwenye hizo ndoa wanaamini ni wao, kweli ukiishi Dar ni sawa sawa na bachelor degree
 
Siku zote ninasema wavulana wa mikoni hamna kitu, na bado watoto wanaozaliwa kwenye hizo ndoa wanaamini ni wao, kweli ukiishi Dar ni sawa sawa na bachelor degree
Inasikitisha sana unanyimwa na akizaliwa mtoto unaambiwa wako na unakubari na unajitangaza kabisa kuwa ninawatoto watatu wakati kupewa papuch hadi selikari iingilie kati dah...!
 
Sasa akikumbuka kichapo ndio akunyime hadi mkalalamike tena mnaiomba selikari iwasaidie kuwaombea mpewe mnatia haibu mikoani
Hapana suala liko hivi ni uchumi tu ndio umekaa upande ila kiuhalisia sisi wa huku tunatakiwa tuwowe walau watatu kwa uchache ili kubalance
 
Back
Top Bottom