Mwanza wahofia kukumbwa na Ebola, wajiandaa kuukabili

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Kutokana na ugonjwa huu kutokea nchi jirani ya Demokrasia ya Kongo, watu wa Mwanza wamehofia ugonjwa huo kufika nchini na Hospitali ya Mkoa imeanza kuchukua hatua sababu ina muingiliano wa watu wa nchi za jirani
Watawaita Jummane wadau wa mkoa kuwapa elimu na kuwaelimisha wananchi mbinu za kukabiliana nao , wananchi wamependekeza pia watu wanaoingia kutoka nchi jirani hasa Mkoa wa Kigoma kuwe na uangalizi

Kwa hisani ya Mwananchi
 
nilikuwa na mpango wa kukimbilia kanda ya ziwa dhidi ya hawa magaidi hapa kibiti sasa nako huko mwanza kunaanza kunuka sielewi sasa pa kukimbilia
 
If anything kills over five million people in next few decades it most likely to be a highly infectious virus rather than a war.

The Ebola outbrake that happened last year in West Africa was a wake up call.

The government must strengthen health system. Where people receive medical care in time.....where a mother delivers safely, a baby gets all the vaccines etc...

This will help to trace diseases in early stages and take control of the spread.

The danger we should really be scared of is not missile it's microbes
 
Serikali itachukua hatua haraka sana
Serikai itaweza wakati haina epidemiologists ambao wapo ready to go?

Ebola ni hatari sana ikiingia sehemu za mjini.

Inaweza ikaondoka na thousands

Hebu fikiria response inavyokuwa ikitokea mlipuko wa kipindupindu. Si kila mwaka tunapoteza watu kadhaa?

Tumejiandaa kweli kukabiliana na tishio la Ebola angali hata international community ilipata taabu kuzuia usisambae?
 
Kutokana na ugonjwa huu kutokea nchi jirani ya Demokrasia ya Kongo, watu wa Mwanza wamehofia ugonjwa huo kufika nchini na Hospitali ya Mkoa imeanza kuchukua hatua sababu ina muingiliano wa watu wa nchi za jirani
Watawaita Jummane wadau wa mkoa kuwapa elimu na kuwaelimisha wananchi mbinu za kukabiliana nao , wananchi wamependekeza pia watu wanaoingia kutoka nchi jirani hasa Mkoa wa Kigoma kuwe na uangalizi

Kwa hisani ya Mwananchi

Tanzania bado hatuna uwezo wa kukabiliana na janga kama Ebola.Tuombe Mungu huu ugonjwa uishie huko huko Congo.

Swali kubwa la kujiuliza, ugonjwa huu husababishwa kwa kula nyama ya panya,nyani,fungo na ngedere.Kwa nini watu hawaaichi hii tabia ya uroho?Tatizo lipo wapi kwa wakongo,waganda na nchi za Africa magharibi?Kwa nini tu waroho kiasi cha kuhatarisha afya zetu pamoja na wote wanaotuzunguka??
 
Usijidanganye kwa kuita watu waroho,ndio utajiepusha na ugonjwa huu!Na kwa akili yako unadhani unaenezwa kwa kula hao wanyama.Kuna watu hawajawahi kula wanyama hao na bado wameugua na kupoteza maisha!Ushukuru Mungu kwa uzima ulio nao na si kutukana watu eti waroho!
 
Acha ukilaza, soma ebola outbreak report ya Liberia ili ujue chanzo chake kikuu ni nini sio kutoa povu.

Unasambazwa kwa njia nyingi hasa kugusana au kushika kitu au mgonjwa ambaye ameshaanza kuumwa ndio maana watu wanashauriwa kunawa mikono yao kila wakati!

Uroho ndio chanzo cha magonjwa mengi hapa duniani kama hujui hilo.Sio wote wanaopata Ebola wanapata kwa kula nyama za pori ila huko ndiko unapotoka kwa uroho wa binadamu!

Kama nimegusa tabia yako ya uroho jirekebishe ili uokoe wengine.Tuendelee kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono yetu kila wakati na kuomba Mungu ugonjwa huu usiingie Tanzania maana hatuna uwezo wa kukabiliana na majanga!!
 
Back
Top Bottom