MWANZA: Tulienda tunachekeana, tunarudi tumenuniana

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Safari ya Mwanza ilikuwa nzuri kweli, nakumbuka brother Lissu , tulipofika alikuwa mchangamfu, hata kwenye kijiwe cha samaki, kama mnavyojua ukifika mwanza lazima kupiga mchemsho wa samaki, kulikuwa na ucheshi na shamlashamla, huku tukibadilishana mawazo na kubeza utumbuaji wa MAGU, kwa kweli tulikuwa na umoja wa hali ya juu kabla ya Jumamosi

Cha kushangaza, leo sina kampani ya kurudi nayo Dar, kila mtu hajulikani kaondokaje au ataondokaje. Wapigania CHAMA tumesikitishwa kwelikweli: tumefungwa, tumevuliwa ngua na polisi, tumechaniwa suti zetu bungeni, tumewekwa sero, wengine mpaka sasa kesi ziko mahakamani kwa ajili ya chama, lakini mwenyekiti kaamua kutupuuza na kumuibua kijana asiye na hata kovu la chama kuwa KATIBU MKUU WETU.

Hali ni tete, wafia chama tunaguna kimyakimya, Huyu Mseminary kweli katuzidi vigezo?? WAKUU ngoja niwahi nipige supu ya samaki pale airport, kabla ndege haijaniacha, make naondoka saa nne leo.

Lakini kila nayempigia HAPOKEI, MAKAMANDA WAKUU wamenuniana huku, kila mmoja anahisi mwenzie ndo kamsnitch, Hata mie nimenuna
 
CCM CCM CCM CCM CCM .....why manahangaika hivi kama mnataka kutaga

All Over ni Malalamiko ya CCM ...Mnalalamika nini kuhusu GS wa CHADEMA

Poleni sana...Lakini subirini kazi
 
Du hawa ndio wale vijana wa Lumumba ambao JK anamkumbusha Kila siku awape ukuu wa wilaya ???? Mañana ndio kazi pekee ambayo yeyote anaweza kuifanya
 
We una uwezo ht wa kupanda ndege kwa ajili ya CHADEMA unalalamika sie ambao tunatembea kwa miguu bado tuna imani na viongozi wetu.POLE
 
Back
Top Bottom