Mwanza: Shinyanga Guest House yaungua moto, Mmliki wake aungua hadi kifo

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
6,525
2,000
Ni hudhuni, masikitiko na furaha hapa jijini mwanza baada ya mzee maarufu na tajiri hapa mjini mzee Shinyanga kufariki jana usiku katika ajali ya moto akiwa katika makazi yake pale shinyanga guest mtaa wa lumumba.
Screenshot from 2017-06-11 11-12-44.png
moja.png

Hii ni Shinyanga Guest iliyoko katika Jiji la Mwanza iliyowaka moto. Mmiliki wake, mzee Shinyanga amefariki dunia ameungua hadi kufa.

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maduhu Masunga maarufu kama mzee Shinyanga (75) amefariki dunia na watoto wake wawili kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyounguza nyumba yake iliyopo mtaa wa Lumumba wilayani Nyamagana, Jijini Mwanza.

Tukio hilo limetokea jana (Juni 10, 2017) majira ya saa 12:30 jioni baada ya moto kuunguza nyumba hiyo na kusababisha uharibifu wa mali na vitu vilivyokuwemo ndani ya nyumba hiyo, kikiwemo kiasi kikubwa cha fedha ambazo hadi sasa thamani yake bado haijafahamika.

Inadaiwa kuwa kabla ya ajali hiyo kutokea, marehemu alikuwa ndani ya nyumba yake akiwa na watoto wake hao wawili na baada ya moto kuzuka, marehemu alikuwa akichukua baadhi ya mali zake ndani ili aweze kutoka nazo nje ndipo kwa bahati mbaya moto ulimzidi na yeye kushindwa kutoka nje na kuungua na moto huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema moto huo ungeweza kudhibitiwa mapema lakini kutokana na miundombinu ya eneo hilo kuwa mibovu ilishindikana kutokana na kuwepo kwa ukuta mkubwa uliopelekea magari ya zimamoto kushindwa kuingia.

Msangi amesema kuwa jeshi la polisi pamoja na jeshi la zima moto kwa kushirikiana na TANESCO wanaendelea kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha moto huo
=============

Anaitwa Maduhu Masunga Lingusha.
Nimefika eneo la tukio na guest house haijaungua.
Kilicho ungua ni nyumba nyingine kwa nyuma ya nyumba ya wageni. Hiyo nyumba iliyoungua kuna watu walikuwa wanaishi pamoja na huyo mzee. Inasemekana moto ulianzia kwenye chumba ambacho kinahifadhi magodoro ambayo ni used na kipo karibu na chumba anacholala mzee. Baada ya moto kuanza moshi mwingi ulitanda na mzee aliitwa akasema anatoka. Lakini watu walishindwa kwenda kumsaidia kwakuwa tayari moshi ulikuwa mwingi sana na kusababisha watu kushindwa kuona. Chanzo cha moto hakijajulikana mpaka sasa. Maelezo nimeyapata kutoka kwa mwanae mmoja wapo wa kiume anayesimamia nyumba ya wageni.
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,251
2,000
Ni hudhuni, masikitiko na furaha hapa jijini mwanza baada ya mzee maarufu na tajiri hapa mjini mzee Shinyanga kufariki jana usiku katika ajali ya moto akiwa katika makazi yake pale shinyanga guest mtaa wa lumumba.
Hebu fafanua hapo kwenye bold mkuu.Furaha itatoka wapi kwenye kifo/msiba?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom