Mwanza: Mtu Mmoja auawa kwa kuchomwa kisu, kisa wivu wa mapenzi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Mtu mmoja amefariki dunia, huku mwingine akijeruhiwa baada ya kuchomwa visu wakati wa ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alimtaja aliyeuawa kuwa ni Makororo Kitota (26) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iloganzala, alichomwa kisu shingoni na kifuani na kupoteza maisha palepale.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu saa nne usiku katika kilabu ya pombe za kienyeji.

Kamugisha alisema mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo alikuwa na ugonvi wa muda mrefu na Kitota akimdhania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe ambaye pia alikuwapo kilabuni hapo wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Agosti 2015 kwa sababu hiyo hiyo kutokana na usaliti katika uhusiano wa kimapenzi.

Aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Nchama Wanda (33), mkazi wa Sabasaba wilayani humo aliyechomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje alipojaribu kuwaamulia wakati wakipigana.

Kamugisha alisema majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi na kwamba, hali yake siyo nzuri.

Alisema mke wa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na polisi baada ya mtuhumiwa na mmiliki wa kilabu hiyo kukimbia kusikojulikana.

Kamanda huyo alisema jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watu hao ili kuwafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
 
Daah hatari saana, poleni wafiwa
 
It is very ikamalaja and ipondason,yaani kapapuchi kalivo kadogo na hata akitumia mwingine kanabaki hivohivo kanasabisha upotevu wa uhai wa mtu mzima!
 
Huyu angekua mwanaume WA dar angekuja jf kuomba ushauri ila Kwa kuwa ni jitu la mkoani linaona limpumzishe in peace

mijitu ya mkoani kwa ujinga

Wanaume wa Dar hawachomani visu kwaajili ya mapenzi.
 
Umri wao wenyewe mdogooooo...na mtauana sana tu kisa K akati siku hizi ukitaka utamiliki hata 10 unawapangia shifti tu.
 
Huyu angekua mwanaume WA dar angekuja jf kuomba ushauri ila Kwa kuwa ni jitu la mkoani linaona limpumzishe in peace

mijitu ya mkoani kwa ujinga

Wanaume wa Dar wanaamini katika Ile slogan kuwa ukiwa mjanja kuchapiwa Ni siri ya ndani.
 
Huyu angekua mwanaume WA dar angekuja jf kuomba ushauri ila Kwa kuwa ni jitu la mkoani linaona limpumzishe in peace

mijitu ya mkoani kwa ujinga
Kwani wa Dar wengi wametokea wap kama siyo mikoani. Wkt mwingine utumie akili kabla ya kupost. Ila siyo tatizo lako bali ni uwezo mdogo wa kufikiri ulio nao
 
MO1kuanzisha li 15759568 said:
Huyu angekua mwanaume WA dar angekuja jf kuomba ushauri ila Kwa kuwa ni jitu la mkoani linaona limpumzishe in peace

mijitu ya mkoani kwa ujinga
We unataka kuanzisha ligi isiyo na kombe
 
Kuchapiwa ni kitu mbaya sana. Yawezekana huyu jamaa ndo alisabisha hiyo ndoa iyumbe! Any way R.I.P .
 
Ugomvi kama huu huwezi kuita WIVU WA KIMAPENZI,bali ni ugomvi wa NDOA,kwa sababu kuna aliyeingilia ndoa ya mtu,
 
Huyu angekua mwanaume WA dar angekuja jf kuomba ushauri ila Kwa kuwa ni jitu la mkoani linaona limpumzishe in peace

mijitu ya mkoani kwa ujinga
Hahaha haka kautani naona kanazidi kupendeza
 
Back
Top Bottom