Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Katibu mkuu Bavicha Julius Mwita ametiwa mbaroni na jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kusalimiana na wanachama wa Chadema kwenye vijiwe kadhaa eneo la Igoma centre jijini humo.
Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde......
UPDATES:
Mkiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Vijana Taifa Patrobas Katambi, Katibu Mkuu wa Vijana Taifa Julius Mwita, Mbunge wa Tunduma Frank Mwakajoka, viongozi wengine wa chama na wanachama wengine, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo cha Polisi Nyakato, jijini Mwanza. Hadi sasa hakuna maelezo ya sababu ya kushikiliwa kwao. Tangu asubuhi Mkiti wa Chama Taifa Mbowe na alikuwa akizunguka katika maeneo kadhaa ya jijini Mwanza kuwasalimia wananchi katika 'vijiwe' mbalimbali jijini humo.
Tumaini Makene
NOTE: Wameachiwa Huru Mdaa Huu saa kuminumbili kasoro dakika ishirini