MWANZA: Majambazi wawili wauawa na Polisi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani Mwanza baada ya kurushiana risasi na askari wakati wakiwa kwenye harakati za za kuvamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini, Baraka Said.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Augustino Senga Alisema katika tukio hilo polisi walikamata silaha moja na risasi 21.

Senga alisema majambazi hao waliokuwa wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 hawajafahamika majina wala makazi yao.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuwapo kwa majambazi yanayokusudia kuvamia kwa mfanyabiashara huyo, tuliweka mtego eneo la tukio ndipo majambazi hayo yalikuja yakiwa kwenye gari jeusi majira ya saa tano usiku,” alisema Senga.

Katika tukio jingine, Wakazi wa stendi mpya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Daudi Joseph (32) na Magashi Mzee wameuawa kwa kupigwa mawe na fimbo na wananchi baada ya kudaiwa kuwatapeli wafanyabiashara wa ng’ombe.

Tukio hilo lilitokea Mei 5, saa saba mchana katika mnada wa mifugo uliopo Kijiji cha Maligisu wilayani Kwimba Mkoa wa Mwanza.

Senga alisema walichukua fedha kwa wafanyabiashara hao wa mifugo wakidai kuwauzia ng’ombe, lakini badala yake walitokomea pasipo kufanya hivyo.

Wakati huohuo, watu wanne wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia duka na kupora fedha ambazo haijajulikana kiasi chake.

Senga alisema tukio hilo lilitokea katika Kata ya Kishiri, wilayani Nyamagana.

Alisema watu hao walivamia duka hilo linalomilikiwa na Phares Grabriel (56).

Senga alisema pia walivamia duka la jirani la Revocatus Phares(28) na kuiba kompyuta mpakato, simu moja na kutokomea na pikipiki.
 
Hongera polisi tunapenda kusikia majambazi yameuawa wakati wa majibizano ya risasi, au yamefia njiani wakati yakiwaishwa hospitali maana tumechoka
 
Si ndio huyo aliyeulizwa na Mwandishi kuwa mbona silaha ni hio hio ambayo wameshaitoa last time kulipokuwa na tukio jingine? Yaani kamanda alienda stoo akatoa silaha ile ile akaja kuwaonoyesha waandishi kuwa ndio silaha iliyokamatwa hahahhahah kumbe jamaa alikua ameshachukua namba zake...
 
Hivi haya matukio ya kurushiana risasi na majambazi kuuwawa yataisha lini? Haki za binadamu naomba ufafanuzi
 
Back
Top Bottom