Derspiegel
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 285
- 242
Lengo siyo kulinganisha Dar na Mwanza isipokuwa kuonyesha kutokuwepo kwa potential city ya kweli ya kuweza kutoa ushindani kwa Dar. Wakati
Hadi kufikia karne ya 15, mji wa kilwa ndio ulikuwa kileleni Afrika Mashariki kwa maendeleo kabla haujaharibiwa na wareno. Wakati wa utawala wa kisultani ni Zanzibar na huku kwetu bara, Bagamoyo ambao ulikuwa mji mkubwa.
Hata hivyo Wajerumani waliuzika mji huo baada ya kuhamishia makao yao mwishoni mwa 1880s katika mji wa Dar na hivyo kupelekea kukua kwa Dar, hasa baada ya ujenzi wa reli ya kati kuelekea kigoma 1905 - 1912). Hata hivyo Wajerumani walikuwa wameshauimarisha mji wa Tanga baada ya kujenga reli ya kupitia milima ya usambara hadi Moshi 1892 - 1912 (kabla ya kipande cha Arusha kuongezwa na waingereza baadaye 1928).
Mji wa Tanga ulizidiwa na Dar kipindi ch waingereza lakini uliendelea kukua kwa kasi kutokana na kilimo cha mkonge na kufanya iwepo tofauti ndogo ya kiushwishi kati ya miji hiyo. Kipindi cha uhuru, Tanga ilipewa hadhi ya manispaa huku Dar ikiwa ni jiji. Hata hivyo, kutokana na kukua kwa kilimo cha pamba baada ya kukamilika junction ya reli ya tabora - Mwanza, (1928), mji wa Mwanza ulikua kwa kasi kipindi hicho hadi wakati wa uhuru na kuupita kwa mji wa Tanga kama mji wa pili kufikia 1978.
Tangu kipindi hicho, Mji wa Mwanza umeendelea kuwa mji wa pili nchini kwa ukubwa, huku ukikua kwa kasi sana miaka ya 1990s na 2000s kutokana na kushamiri biashara ya samaki. Hata hivyo, kulinganisha na zamani, jiji la Dar lumekuwa likiongezeka kwa kasi na kuiacha kwa mbali miji mingine, licha ya jiji la Mwanza pia kukua kwa kasi. Hata hivyo kudorora kwa biashara ya sangara, kumepunguza kasi ya ukuaji ya jiji hilo ambalo kwa miaka ya 1990 na 2000s lilikuwa miongoni mwa miji inayokua kwa sana barani Afrika.
Kwa sasa, kuna miji mingine inayokua kwa kasi nchini, ikiwemo Dodoma, Mbeya, Arusha, Mtwara na baadaye kidogo Tanga (mafuta ya Uganda). Lakini ukiacha jiji la Tanga na Mbeya, hakuna jiji lingine nchini litakalokuwa that much stable kuzidi jiji la Mwanza kutokana na potentiality ndogo ya miji mingine.
Mfano jiji la Arusha (ufinyu wa maeneo na kuzungukwa na wilaya na mikoa kame kila kona) na Manispaa ya Dodoma (ukame)