Mwanaume yupi mwoga wa kumkosa mwenzi wake kati ya hawa wawili?

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,488
Wadau tusaidiane hapa kwa mtazamo wako unahisi ni mwanaume yupi alikuwa mwoga kumpoteza mwenza wake kati ya hawa wawili?

Mwanaume "A" alikuwa na mahusiano na mpenzi wake kwa muda mrefu. Alipojitokeza kwa wazazi na ndugu na kujitambulisha, ilichukua miezi 6 kufuata hatua zote halali hadi kufunga ndoa.

Mwanaume "B" yeye alimpa mpenzi wake mimba na kuanza kuishi nae hadi amezaa mtoto na ameanza shule ila bado hawajafunga ndoa.

Sasa kulikuwa na ubishi kati ya "A" na "B" kila mmoja akimwambia mwenzake kuwa wewe ni mwoga wa kukosa mke ndo maana ukafuata njia uliyofuata.

Kati ya "A" na "B" yupi mwoga? Kwanini?.
 
Back
Top Bottom