Mwanaume kuhonga ni sahihi...

Mwanaume kuhonga ni sahihi...

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
40,355
Reaction score
62,596
Huwa najiuliza kwa nini mwanaume amewekwa kwenye nafasi ya kumhonga mwanamke ili aweze kutimiza mahitaji yake ya kimahusiano,je ni sahihi kuwa hivyo?Na kwa nini isiwe kinyume chake?Au wanaume ndio wenye hisia kali sana za kumhitaji mwanamke zaidi ya wao?Tujadili...
 
Nadhani huu mjadala tusiuhadili maana hauna muafaka...

Miongoni mwetu kuna wanaohongwa, wanaohonga, wanaohongana na wasiohongwa wala kuhonga.

Kila mmoja aendeshe mahusiano yake aonavyo.
 
ha ha ha ha weka maoni yako mkuu
 
ha ha ha ha weka maoni yako mkuu
Mkuu hongo ni suala mtambuka....unaweza kuitoa pasipo hata kujua.

Ukisogelewa kidogo ukapapaswa kifua unasahau mjadala. Mimi wanachonikera tu wengi ni kupendea hongo basi.
 
ha ha ha ha nahisi pia, wanatumia udhaifu wetu ili kufanikisha mambo yao;kwa hiyo inamaanisha wao bila hongo hawapatwi na hisia?
 
Hapo sijajua mkuu....tafadhali usinigombanishe nao...nisije nikanyimwa salamu PM.
 
Kuna mmoja weekend hii baada ya kumaliza shows zetu akaona asisitize kabisa kuwa "uwe unanitunza!".

Nilibaki nacheka kibaharia tu.

Yaani kuonana inakuwa kama nakununua alafu bado nikutunze!
 
ha ha ha ha hatari hiyo
 
Jibu lipo hapa Mwanzo 3 : 1-20
Na WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha.
Fikra hizi walizonazo wanaume kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
 
Kuna ukweli,nadhani huwa wanatanguliza kwanza kuwa na uhakika wa kiuchumi kama chaguo la kwanza,na la pili baada ya kukamilisha la kwanza ni namna ya kutuliza hisia zake.
 
Back
Top Bottom