Mwanaume kama huna kizazi, katu usije kujaribu kumwambia mkeo atembee nje ya penzi lenu

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,397
9,246
Wasalaam wakuu,

Bila shaka wengi wetu tumeshashuhudia Wanaume wengi walioko kwenye ndoa ambao hawana Uwezo wa kuzalisha na kisha kuwaambia wake zao watafute wanaume nje kwa siri ili wapewe mimba.
Wengi waliotumia njia hii ndoa zao zimevunjika kwa sababu mke anakuwa hana tena Upendo wa wewe na kisha kuhamishia kwa yule aliyempa mimba.
Ni vema kama wewe upo kwenye ndoa na tayali Daktari kathibitisha huna uwezo wa kumpa mke mimba ni bora Umpe talaka muachane kwa Amani kuliko kumwambia eti atafute kijana kwa siri ampe mimba na kisha kumlipa yule kijana kisha kumwambia asiwajue! Kwa hapa mwanaume utakuja kulia machozi ya kamasi. Au ni bora muachane halafu wewe utafute tu Mwanamke ambaye ni Single Parent na umuoe umlele watoto ambao wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwako.
 
Eeheee....Imetokea Kwako Ama? Naona Msisitizo Kweli!!
Naweza nikakubali na usiweze kuamini lakini pia naweza nikakataa na usiweze kuamini.
Wengine humu ndani tulisha jukuu kwa kwa hiyo tunachofanya ni kuyatoa yale tulioyaona huko nyuma ambayo yanarudiwa leo kwa njia zile zile..
Kikubwa angalia yaliyomo kama yanakufaa au la!!
 
Hahahaha unafunguka tu ili mjue jinsi ya kusolve mambo mengine yanatibika
 
Nimeshuhudia jambo kama hilo ila mwanamke aliendelea kumpenda mume wake na wakapata watoto wawili wa nje na hadi leo hii ndoa yao bado iko imara
Ni wachache sana wa hivyo, Wa kwanza nilimshudia mwaka 1988 alifanya hivyo hivyo lakini baadaye mke akahamia kwa baba wa mtoto na wa pili ni wiki iliyopita nae alifanya hivyo hivyo na sasa baba wa mtoto amechachamaa anataka mtoto wake.
 
Wasalaam wakuu,

Bila shaka wengi wetu tumeshashuhudia Wanaume wengi walioko kwenye ndoa ambao hawana Uwezo wa kuzalisha na kisha kuwaambia wake zao watafute wanaume nje kwa siri ili wapewe mimba.
Wengi waliotumia njia hii ndoa zao zimevunjika kwa sababu mke anakuwa hana tena Upendo wa wewe na kisha kuhamishia kwa yule aliyempa mimba.
Ni vema kama wewe upo kwenye ndoa na tayali Daktari kathibitisha huna uwezo wa kumpa mke mimba ni bora Umpe talaka muachane kwa Amani kuliko kumwambia eti atafute kijana kwa siri ampe mimba na kisha kumlipa yule kijana kisha kumwambia asiwajue! Kwa hapa mwanaume utakuja kulia machozi ya kamasi. Au ni bora muachane halafu wewe utafute tu Mwanamke ambaye ni Single Parent na umuoe umlele watoto ambao wanaweza kuja kuwa msaada mkubwa kwako.
Hii kitu sio rahisi kama unavyofikiria ww.,Pia ni ngumu sana kwenda kwa mwanamke mwenye watoyo wake ukamlee watoto wasio wako...,Huu mchezo hauhitaji hasira....,
 
Nimeshuhudia jambo kama hilo ila mwanamke aliendelea kumpenda mume wake na wakapata watoto wawili wa nje na hadi leo hii ndoa yao bado iko imara
Huu mchezo hauhitaji hasira.,likikujuta hili balaa ni lazima ukubali matokeo na uwe mpoleeeeee
 
Haya mambo hua naombaga sana Mungu aniepushie....na nikiona mtu mwenye shida ya namna hyo kamwe siwezi mdharau/kejeli. Hujafa hujaumbika.

Hata posting hapa nimejikaza sanaa. Daah ila Mungu ni mwaminifu atawapatia hao wanandoa furaha kwa wakati wake. Tumuamini.
 
hii kama mwanamke anakupenda na kukuheshimu ataiba mwenyewe bila kumjulisha huyo mwanaume mwingine.
atakachofanya ni kumtegeshea tu jamaa aaafu uhusiano unakatika. akitoka hapo wasijuane. ila shida ni pale ambapo utamuudhi na kumtibua. akamwambia na mtoto kuwa huyu sio baba yao.
ila ukiwa na hela yote yanawezekana.
 
Back
Top Bottom