Mwanasiasa mpe fedha au madaraka

Administer

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
707
1,000
Ukitaka kujua msimamo wa mwanasiasa au mtu mwingine yeyote apate majaribu kwanza.Hata mimi ninayeandika ukitaka kujua msimamo wangu katika jambo fulani nipe majaribu.

Sijui ni Tanzania tu au na kwingineko haya yanatokea.Unaweza kumsikiliza mwanasiasa fulani kwa misimamo yake,ukajiridhisha kweli huyu ana msimamo. Anaweza kuwa ni mpinga rushwa mkubwa na mnyenyekevu mkubwa katika chama na viongozi wake. Akipata majaribu anashiriki katika rushwa, anahamia kwenye chama ambacho kila siku alikua nahubiri ni chama cha watenda maovu.

Majaribu yenyewe ninayozungumzia hasa fedha au madaraka .Wanasiasa wengi wapo kwenye siasa kwasababu ya matumbo yao. Ukimsikia akisema tupo kwa ajili ya kuwatetea au kulinda maslahi ya watanzania uyue mtanzania wa kwanza ni yeye na familia yake
 
Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
1,605
2,000
Siasa ni ajira kama zilivyo ajira nyingine. Usitegemee makubwa kutoka kwa wanasiasa. Chagua mwanasiasa atakayelinda maslahi yako. Ukiona hakuna nenda wewe kagombee.

Maendeleo yanayoletwa na mwanasiasa ni kwa lengo la kupata kura na kula kwa awamu nyingine. Akishiba na kusaza hawezi kamwe kumsikiliza mtu. Pia mwenye njaa sana sharti ashibe yeye na familia yake, wengine hadi ukoo ndio kidogo awafikirie wengine.

Uongozi ni karama. Sio kila mwanasiasa ni kiongozi.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
21,252
2,000
Si mwanasiasa tu hata mkeo tabia yake halisi utaijua siku akishapata pesa, iwe pesheni au hata kama ni pesa ya mgawo wa urithi kwao.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,562
2,000
Ukitaka kujua msimamo wa mwanasiasa au mtu mwingine yeyote apate majaribu kwanza.Hata mimi ninayeandika ukitaka kujua msimamo wangu katika jambo fulani nipe majaribu.

Sijui ni Tanzania tu au na kwingineko haya yanatokea.Unaweza kumsikiliza mwanasiasa fulani kwa misimamo yake,ukajiridhisha kweli huyu ana msimamo. Anaweza kuwa ni mpinga rushwa mkubwa na mnyenyekevu mkubwa katika chama na viongozi wake. Akipata majaribu anashiriki katika rushwa, anahamia kwenye chama ambacho kila siku alikua nahubiri ni chama cha watenda maovu.

Majaribu yenyewe ninayozungumzia hasa fedha au madaraka .Wanasiasa wengi wapo kwenye siasa kwasababu ya matumbo yao. Ukimsikia akisema tupo kwa ajili ya kuwatetea au kulinda maslahi ya watanzania uyue mtanzania wa kwanza ni yeye na familia yake
Wanasiasa hata ukiwapa mbunye Wana change mind completely
 
guwe_la_manga

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
2,074
2,000
Hata Tundu Lissu nae tusimuamini?
Ukitaka kujua msimamo wa mwanasiasa au mtu mwingine yeyote apate majaribu kwanza.Hata mimi ninayeandika ukitaka kujua msimamo wangu katika jambo fulani nipe majaribu.

Sijui ni Tanzania tu au na kwingineko haya yanatokea.Unaweza kumsikiliza mwanasiasa fulani kwa misimamo yake,ukajiridhisha kweli huyu ana msimamo. Anaweza kuwa ni mpinga rushwa mkubwa na mnyenyekevu mkubwa katika chama na viongozi wake. Akipata majaribu anashiriki katika rushwa, anahamia kwenye chama ambacho kila siku alikua nahubiri ni chama cha watenda maovu.

Majaribu yenyewe ninayozungumzia hasa fedha au madaraka .Wanasiasa wengi wapo kwenye siasa kwasababu ya matumbo yao. Ukimsikia akisema tupo kwa ajili ya kuwatetea au kulinda maslahi ya watanzania uyue mtanzania wa kwanza ni yeye na familia yake
Uko sahihi
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
3,934
2,000
Siasa ni ajira kama zilivyo ajira nyingine. Usitegemee makubwa kutoka kwa wanasiasa. Chagua mwanasiasa atakayelinda maslahi yako. Ukiona hakuna nenda wewe kagombee.

Maendeleo yanayoletwa na mwanasiasa ni kwa lengo la kupata kura na kula kwa awamu nyingine. Akishiba na kusaza hawezi kamwe kumsikiliza mtu. Pia mwenye njaa sana sharti ashibe yeye na familia yake, wengine hadi ukoo ndio kidogo awafikirie wengine.

Uongozi ni karama. Sio kila mwanasiasa ni kiongozi.
👊👊
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom