Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
CSR (Cooperate Social Responsibility) - maana yake ni vile vitengo maalum vinavyoundwa na makampuni makubwa vyenye dhumuni la kutenga fedha kwa ajili ya kushughulika moja kwa moja na shida nyingi za jamii.
Ulimwengu wa ushindani wa kibepari ndio huu tunaoishi sasa. Lakini pamoja na falsafa zinazosema kwamba ubepari ni unyama, bado huo huo mfumo dhalimu unaziangalia jamii nyingi zenye pato dogo, ambazo zinahitaji kunyanyuliwa. Mfumo huu huu dhalimu unatenga fedha kwa ajili ya wanajamii wenye mahitaji mbalimbali.
Binafsi sipendezewi na dharau zinazozidi kushika kasi kwenye jamii ya kitanzania. Kuna maneno ambayo kwenye miaka ya hivi karibuni, yanaonekana ni ya kawaida lakini yanabeba kila aina ya sumu inayoishi ndani kabisa ya dharau. Kuna maneno kama vile "wala viwavi", haya ni kielelezo cha watu kujitojitambua, kutojifahamu. Ni maneno yenye kuwakilisha jamii zinazoishi kibinafsi sana. Dhana nzima ya CSR kwenye miaka ya sasa, ni kupunguza ule unyama na majivuno yanayokuwepo wakati jamii fulani inapokuwa imefanikiwa lakini kuna jamii nyingine nyingi tu ambazo bado zina maisha duni.
Watanzania wenzangu haswa wale waliobahatika kupata elimu ya juu, jamani chonde chonde, dharau huwa ni chanzo cha laana kwenye nchi fulani. Hawa wananchi wanaodharauliwa na kukejeliwa kwa sababu ya uduni wa maisha yao, ndio hao hao ambao watu wa mijini wanapofariki dunia, wanakuwa wa kwanza kutoa ushirikiano katika kuhakikisha miili yao inahifadhiwa kwa heshima zote huko vijijini ambako ni asili yetu sote.
Nitamuheshimu sana mwanasiasa yoyote yule ambaye amebahatika kupata elimu ya juu, lakini bado anaishi na moyo wenye CSR daima. Moyo ulio tayari kujishusha kwa ajili ya wananchi wengi wa nchi hii ambao bado ni masikini.
Ukiangalia takwimu nyingi zinazohusiana na ubora wa maisha utagundua kwamba wanaotukanwa na wale wenye elimu kubwa ni wengi kuliko hao wanaojiona ni bora. Tazama uwiano wa daktari moja anatibu wagonjwa wangapi. Tazama mwalimu mmoja darasani anafundisha wanafunzi wangapi. Tazama asilimia ya watu wenye uwezo wa kuweka umeme majumbani mwao. Tazama mambo mengi, utagundua kwamba hizi mbwembwe za wenye elimu kubwa ni za kijinga.
Nitamuheshimu sana mwanasiasa ambaye anatumia nguvu kubwa kuieleza jamii juu ya ukweli kwamba CSR haiwezi kupoteza maana na umuhimu wake.