DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema anashangazwa na kauli ya “No reforms, no election” ikizingatiwa kuwa mabadiliko ya kisheria yaliyopendekezwa na vyama vya siasa tayari yamefanyika.
Akizungumza leo Jumamosi Juni 21, 2025, kwenye kongamano la kwanza la kitaifa la kisheria lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam, Johari amesema mageuzi hayo yamefanyika kupitia mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai.
Ameeleza kuwa mapendekezo hayo yalijumuisha kutungwa kwa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi, kuunganisha sheria ya uchaguzi wa Rais na serikali za mitaa mchakato uliokamilika mwaka 2024 na kuboresha Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuimarisha ushiriki wa makundi maalumu.
"Yote haya yametekelezwa kutokana na maoni ya vyama vya siasa. Sasa mtu anaposema ‘No reforms, no election’, inashangaza, kwa sababu reforms zimeshafanyika,” amesema Johari.
Mgeni rasmi katika kongamano hilo linaloendelea ni Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
Ikumbukwe kuwa kwa takriban miezi minne nyakati tofauti, Chadema kimekuwa kikinadi kampeni yake ya No reforms, no elections’ nchi nzima kikishinikiza kufanyika kwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi, kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.
Chanzo: Mwananchi