Mwanasheria IPTL acharuka

Mwanasheria IPTL acharuka

Fikiri Kisomi

Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
5
Reaction score
1
Mwansheria na Katibu wa Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Kampuni ya Pan African Power (PAP), Joseph Makandege amesema baadhi ya watu wanaichafua IPTL kwa sababu zao binafsi, huku ukweli ukifichwa.
Makandege alibainisha kuwa, baadhi ya watu wanatumiwa kuichafua IPTL huku akisisitiza kuwa, ipo siku ukweli wake utafahamika. Alisemaa wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kueleza ukweli halisi, lakini umekuwa ukipotoshwa kwa maslahi binafsi ya watu.

Pia, alizungumzia zaidi ya sh. bilioni 1.6 alizopata Waziri wa Ardhi, Nyumba an Maendeleo ya Makazi, Prf. Anna Tibaijuka kutoka kwa mmoja waliokuwa wanahisa wa IPTL, James Rugemalira kuwa, hazihusiani na fedha za Escrow.
Mwansheria huyo alisema fedha hizo zilikuwa ni mali ya Rugemalira, ambaye wakati akizitoa kwa Tibaijuka, hakuwa tena mwanahisa wa kampuni hiyo.

"Rugemalira aliuza hisa zake zote na kufuata taratibu za kisheria na nyaraka zipo ofisini kwetu na Brela. Rugemalira hakulipwa fedha za Escrow, bali alilipwa fedha za kuuza hisa zake," Alisema.
Makandege aliongeza kuwa: "mtu mwenye fedha zake kaamua kumpa mtu mwingine ama kwa kumkopesha, kumsaidia au kwa mapenzi yake mwenyewe, shida iko wapi na IPTL inahusikaje hapa. Nafikiri Rugemalira ndiye anayejua matumizi ya fedha zake.
"Izingatiwe kwamba, fedha za Escrow si hisani wala rushwa ni malipo halali yanayotokana na IPTL kuwauzia Tanesco umeme, ambao Watanzania wameutumia na wanendelea kuutumia. Je, wanasiasa walitaka tuwape umeme bure" alihoji.
Makandege alisema IPTL/PAP ni mmiliki halali aliyefuata taratibu zote na malipo aliyopewa kutoka akaunti ya Escrow ni halali na hakuna vitendo vyovyote vya ufisadi.
"Umma utaelewa suala hili, wanaozungumza wanatumiwa kwa kuwa IPTL/PAP ndiyo kampuni inayoiuzia umeme kwa bei nafuu Tanesco kuliko kampuni zote na kinachofanyika ni wivu wa biashara", alisema.

Chanzo: Jambo Leo, Sauti ya Jamii; Septemba 21- Ukurasa wa 1 & 4
 
Mwakandeke,mujiriwa wa idara ya mahakama,kaacha kaenda chuo kikuu dar es salaam,baadae kaajiriwa TRA,anyway, IPTL itafute afisa uhusiano,au mwakandenge ana~play double role
 
Ila kuna watu wana fedha mbaya dah, maisha hayo bongo hapo shida, wengine wanapeana msaada(zawadi) ya bilioni 1.6.mchana kweupeee, kweli shida, usipokuwa makini unaweza kumkufuru mungu..
 
Jamani mama wa watu Tibaijuka, alishatukanwa mpaka basi. kumbe kaonewa! I think, people have to come back and apologise for this mama.
 
Ila kuna watu wana fedha mbaya dah, maisha hayo bongo hapo shida, wengine wanapeana msaada(zawadi) ya bilioni 1.6.mchana kweupeee, kweli shida, usipokuwa makini unaweza kumkufuru mungu..
Mkuu walifanya kazi kwa bidii wakati wa ujana wao, sasa nyie mnashinda kwenye vijiwe kila siku utapataje maisha mazuri?
 
Hahahahaha lol!!! Mbona mama baada ya bomu kulipuka aliweka hadharani katika jitihada zake za kujisafisha kwamba hakujua kama pesa zile zina mushkeli!!! Sinema ya kumsafisha fisadi Tibaijuka imeanza rasmi!!
 
Si asubiri uchunguzi kukamilika badala ya kuja na maelezo haya ya malalamishi ambayo hayatabadilisha mawazo ya watu kuhusu deal hili.
 
Mkuu walifanya kazi kwa bidii wakati wa ujana wao, sasa nyie mnashinda kwenye vijiwe kila siku utapataje maisha mazuri?
kufanya kazi kwa bidii ni kuweka michongo ya kuiba benki kuu sio..?
 
Back
Top Bottom