Mwanasheria CHADEMA Mabere Marando, apelekwa India kwa matibabu

Mwanasheria CHADEMA Mabere Marando, apelekwa India kwa matibabu

Bukanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
2,857
Reaction score
1,938
marando-300x294.jpg

Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando, amepelekwa nchini India na familia yake kwa ajili ya kupata matibabu zaidi -- yameripoti magazeti la MTANZANIA na MAJIRA siku ya Jumanne, Septemba 15, 2015.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Steven, alisema Marando aliondoka juzi na baadhi ya ndugu zake.

"Wameondoka Jumapili kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi, wenyewe walisisitiza tusitaje ugonjwa unaomsumbua ndugu yao, na kwamba ataeleza mwenyewe (Marando) pindi atakapopona"

Marando ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA, alifikishwa hospitalini hapo usiku wa Septemba 7, mwaka huu, baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake na kuazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete karibu wiki nzima kwa ajili ya matibabu.

=================================

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CHADEMA ambaye pia ni Mwanasheria maarufu nchini, Mabere Marando aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), kwenye Taasisi ya Moyo, amepelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wahospitali hiyo, John Stephen, alisema Marando aliondoka nchini juzi; na akiwa nchini humo, atapatiwa matibabu ya maradhi yanayomkabili.

Alisema Mabere aliondoka hospitalini hapo akiwa katika hali mbayakiafya, hivyo wanaamini afya yake itaimarika baada ya kuanza kupatiwa matibabu akiwa nchini humo.

Marando alilazwa hospitalini hapo usiku wa Septemba 6, mwaka huuna alichukuliwa vipimo mbalimbali ili kujua tatizo linalomkabili, lakiniwauguzi hawakuwa tayari kusema alikuwa anasumbuliwa na maradhi gani kwa sababu wao si wasemaji wa familia
.
Chanzo: Majira
 
Get well soon! Mimi nafikiri amekolimbwa kwa sababu alisema kuwa atatangaza matokeo ya uraisi kabla ya nec
 
Nina wasiwasi na kuugua kwa huyu mwanasheria, kuna kila dalili ya mchezo mchafu, anyway namtakia afya njema na uponaji wa haraka.
 
ALLAH ni muweza wa kika kitu.Anayajuwa yote yaliyo nyuma yetu na mbele yetu.
 
Daktari wanatibu lakini Mungu pekee ndiye anayeponya
 
Apone mapema aje kutangaza matokeo kabla ya tume
 
Kwanini iwe baada ya kutueleza atatutangazia matokeo siku ya pili tu
 
Tunakutakia uponaji wa haraka mwanasheria Marando!
 
nanusa harufu ya kazi mbaya ya wanamtandao (lowasa,rostam,patel et al) kumfanyia yale waliomfanyia mwakyembe baada ya sakata la richmond bungeni.
huyu alikuwa hakubaliani kwa dhati na ujio wa lowasa kwenye vyama vya upinzani.
pole sana marando. jini limevamia vyama vya upinzani, wataumia wengi zaidi
 
kijana chunga maneno yako na uache hizo kauli za utata mara moja!
 
nanusa harufu ya kazi mbaya ya wanamtandao (lowasa,rostam,patel et al) kumfanyia yale waliomfanyia mwakyembe baada ya sakata la richmond bungeni.
huyu alikuwa hakubaliani kwa dhati na ujio wa lowasa kwenye vyama vya upinzani.
pole sana marando. jini limevamia vyama vya upinzani, wataumia wengi zaidi

Lisemwalo lipo!Alionya ccm ikimteua lowasa Chadema watamwaga siri nzito za lowassa.
 
Mi hata skumbuki tupo season/episode ya ngapi jamani anayefatilia.

Haya acha tu tutazame hivyo hivyo cha msingi series iishe tu kabla umeme haujakatika.
 
nanusa harufu ya kazi mbaya ya wanamtandao (lowasa,rostam,patel et al) kumfanyia yale waliomfanyia mwakyembe baada ya sakata la richmond bungeni.
huyu alikuwa hakubaliani kwa dhati na ujio wa lowasa kwenye vyama vya upinzani.
pole sana marando. jini limevamia vyama vya upinzani, wataumia wengi zaidi

Mkuu upo sahihi huyu alishakuwa sumu kwao..mwezi wa saba aliripotiwa akisema kwamba ana mengi mabaya ya kueleza juu ya Lowasa..hii ya kuuguwa gafla inatupa ukakasi kidogo
 
jamaaa si alisema atatangaza matokeo au ndio kushugilikiwa huko?

alisema anayo mengi ya lowassa, na wanakaa kimya kwanza kuwaachia kina nape na makonda kufanya kazi hiyo. Lakini makombora yake yako spare, alafu huyu bw ana msimamo kama dr slaa, duh inashtua sana
 
nanusa harufu ya kazi mbaya ya wanamtandao (lowasa,rostam,patel et al) kumfanyia yale waliomfanyia mwakyembe baada ya sakata la richmond bungeni.
huyu alikuwa hakubaliani kwa dhati na ujio wa lowasa kwenye vyama vya upinzani.
pole sana marando. jini limevamia vyama vya upinzani, wataumia wengi zaidi
Mwakyembe anaugua ugonjwa fulani... File lipo ikulu la report ya daktari...
 
Back
Top Bottom